15 June 2011

Wanafunzi 400 watimuliwa UDOM

Na Waandishi Wetu

SIKU moja baada ya serikali kutangaza kukubali kuwalipa posho ya mafunzo kwa vitendo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), uongozi wa chuo hicho
umewatimua wanafunzi takriban 400 kwa kuchochea mgomo.

Hatua hiyo ilifikiwa jana saa 10 jioni baada ya uongozi wa chuo hicho kudai kubaini njama za wanafunzi hao kushawishi wenzao kufanya mgomo kutaka kuvuruga ratiba ya mitihani kuanzia Juni 20, kuwapiga wenzao, na kuvunja mlango wa darasa la kitivo cha sayansi asilia.

Wakizungumza na Majira kutoka chuni hapoa jana, baadhi ya wanafunzi walisema hali ni tete katika eneo hilo na kwamba waliofukuzwa sasa wamekuwa mwiba mkali kwa wenzao huku wakizuia daladala kufika katika eneo hilo kwa madai kuwa ingewezesha kuwaondoa wakati wakitaka washinikize serikali kuwasikiliza kwanza.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula, alisema wamefikia hatua ya kuwafukuza wanafunzi hao ambao wengi wao ni wa mwaka wa pili wanaochukua kosi ya Ushirikiano wa Kimataifa kutokana na kuonekana kuwa vinara wa mgomo.

"Haya mambo ya kuwapiga wenzao, kutaka kuchochea vurugu wamenza tangu mchana, wameng'oa miti tuliyopanda hapa chuoni, wanawapiga wenzao wanaoingia darasani na wamevunja mlango wa darasa.

Hatuwezi kuacha kufanya fujo hivi katika eneo la taaluma, lakini kibaya zaidi serikali imeshatoa tamko, serikali ilinituma mimi jana usiku na kueleza kuwa imekubali itatoa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na kwao hapa UDOM ni special case (suala mahususi), lakini hawakusikiliza," alisema Prof. Kikula.

Alisema juzi usiku alifanya mazungunzo na viongzoi wa wanafunzi hao na kuwaomba wakawajulishe wenzao huku wakishinikiza Waziri wa Elimu, Dkt. Shukuru Kawambwa kutoa majibu hayo mbele ya wanafunzi wote huku dalili zikionyesha si salama.

"Mhe Dkt. Kawambwa alikuja akazungumza na viongozi wa wanafunzi na tukawapa taarifa kwamba pelekeni ujumbe kwamba serikali imekubali, sisi baada ya kuona watu wanapigwa hatuwezi kuruhusu hali kama hiyo na wale vinara tunawaondoa, ni wale wa mwaka wa pili wa International Relation, wote waliokamatwa na polisi jana (juzi) wakiandamana, walivunja sheria na wote waliochochea, tumewaondoa jumla yao kama 400 hivi," alisema Prof. Kikula.

Alipoulizwa hatua zitakazochukuliwa na chuo kuhakikisha wanafunzi hao wanaondoka kutokana na taarifa kwamba wamegoma kufanya hivyo na wanatafuta uwezekano wa kupata ushirikiano kutoka kwa wenzao alisisitiza kuwa lazima waondoke.

"Sisi tusingependa kufikia hatua ya kuwaondoa lakini kwa kuwa wameshafikia pabaya ni lazima waondoke tu, hata kama hawataki, tutawaita mmoja mmoja kuja kujitetea ambaye utetezi wake utaridhisha atarudi, ila kwa sasa lazima waondoke ili tufanye mtihani wetu kama ilivyopangwa," alisema.

Alisema fedha hizo zitaingizwa na serikali kabla ya muda wa kuanza mafunzo hayo na kwamba kwa mujibu wa maelezo serikali ilikubali kuchukua jambo hilo mahususi kuhakikisha wanafunzi hao wanaendelea na masomo bila kukwama.

Kauli ya Waziri Kawambwa

Siku moja baada ya wanafunzi wa UDOM, kuandamana wakitaka kupatiwa mafunzo kwa vitendo kozi zote ambazo hazikuwekwa kwenye utaratibu huo serikali imekubali madai yao na kuanzisha mpango wa mpito utakaowawezesha kupata mafunzo hayo kuanzia mwaka huu wa masomo.

Mpango huo wa mpito utawasaidia wanafunzi wa Chuo cha Sanaa na Sayansi Jamii na Skuli ya Sayansi Asilia na Hisabati chuoni hapo ulikubaliwa kwa pamoja na serikali pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Mpango huo pia utazithamini rasimu za mitaala ya kozi hizo na kufanyiwa kazi zaidi ili zifikie viwango vya kukubalika kuwa na mafunzo kwa vitendo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo Stadi, Dkt. Shukuru Kawambwa, alisema wanafunzi hao na wengine nchini watapata fedha zao kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo mapema kabla hawajaanza baada ya mhula wa mwaka wa masomo 2010/2011 kumalizika.

Alisema wanafunzi wa Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii na Skuli ya Sayansi Asilia na Hisabati UDOM walifanya maandamano kudai wanafunzi wote katika program zote 13 za chuo hicho ambazo hazikuwa na mafunzo kwa vitendo waingizwe katika utaraitibu huo.

Alisema TCU imefanya tathmini ya rasimu za mitaala iliyowasilishwa na kubaini kuwa programu hizo zinatakiwa kufanyiwa kazi zaidi ili ziweze kufikia kiwango cha kuweza kukubalika kuwa mafunzo kwa vitendo na kwamba serikali imebaini kuwepo kwa hitaji la kutoa miongozo katika eneo la mafunzo kwa vitendo ili kuweka utaratibu wa mafunzo hayo utakaotumiwa na vyuo vikuu vyote nchini.

Alisema pamoja na TCU kuwasilisha maamuzi yake serikali kwa kutumia busara zaidi imeamua kuwa na mpango wa mpito ambao utawawezesha wanafunzi hao kufanya mafunzo kwa vitendo katika mwaka wa masomo
2010/2010.

23 comments:

  1. serikali isidanganye uma kozi hizo 13 walikua na mafunzo kwa vitendo tangu awali lakini zipo kozi nyingine wamekataliwa kabisa kwenda mafunzo kwa vitendo. mwana UDOM

    ReplyDelete
  2. Sikweli kwamba wanafunzi wa International relations ndio vinara wa mgomo. Uongozi wa chuo una asume hivyo kwa vile wanafaunzi hao wa mwaka wa pili ambao jumla yao ni 374, ndio pekee ambao chuo kilisema kwamba hwawezi kupatiwa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa vile hahwajaandaliwa mahali pa kufanyiwa hayo mafunzo ya vitendo. Waliowashinikiza kwamba wasiondoke ni waanafunzi wa kozi zingine. Inabidi Uongozi ufanye uchunguzi wa kina kabla ya kutoa kauli za upotoshaji wa hali alisi ya ukweli.

    ReplyDelete
  3. Makamu Mkuu wa chuo anudanya umma. Wanafunzi wa International relations sio waliongoza mgomo huo. Ni wanafunzi wa kozi nyingine!

    98% ya wanafunzi wote wa mwaka wa pili wa international relations hawakuingizwa ktk program ya kupatiwa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa sababu wanazozijua viongozi wa chuo. Labda hii ndiyo cause ya assumption hiyo kwamba ndio vinara wa mgomo! Prof. Kikula angefanya utafiti kwanza kabla ya kutoa hizo accusations zake.
    Hawatendei haki wanafunzi hao kama mlezi wao mkuu hapo chuoni.

    ReplyDelete
  4. timua wajinga hao kodi zetu wenyewe halafu bado wanaharibu mali na hata miti wanang'oa wakafanye hivyo makwao, wengi wa watoto hao bilashaka ni wa walala hoi na bilashaka ujinga wao unapelekea kufanya upumbavu huo. Sawa sawa hatua zilizochukuliwa mtaka cha uvunguni?

    ReplyDelete
  5. Wahuni wapo mpaka vyuoni sasahivi, umbumbu wao wa kutokufikiria na kuchambua manbo ndio uliowafikisha hapo, wengi wao wanafuata Mkumbo tu, hawajui nini wanachotakiwa kufanya katika level hiyo waliyofikia, na wengi wa wanafunzi hao ni wa walala hoi, labda ndiyo inayopelekea kuingia kwenye vurugu hizo kirahisi kwa kuwa wanataka kuchakachua maisha mapema, Nakipongeza Chuo na ninashauri Wawe makini na wawachuje ili kupata hiyo Cream iliyozalisha mgomo huo na kusababisha hasara kubwa, angalia walivyo na akili finyu hata Miti wanaiharibu tena iliyopandwa hivi karibuni kwa nguvu kubwa na gharama kubwa naDodoma ikichukuliwa ni nusu Jangwa. Fukuza mtu anavuna alichopanda.

    ReplyDelete
  6. Chadema Oyeee!!! mnaona sasa ushawishi wenu? Chadema Mnaona lakini? sasa tunasema hivi tutaanza kuwapiga mawe mkija vyuoni. Tumekwisha wachoka kilasiku Uchochezi tu. sasa tunafukuzwa kwa Posho zenu Shs 20,000 tu zimetuponza. Mh Freeman waambie kabisa watumishi wako Lema, Mdee, Zito na huyo aliyeshindwa Segerea tutawaumiza wasije tena Vyuoni. hasa hapa UDOM

    ReplyDelete
  7. Safi sana Uongozi wa UDOM. kama siku zote mngelikuwa serious kiasi hiki nidhamu ingekuwa juu. hasa hapo Udom sijui wanaingia watoto wa aina gani hapo bilashaka ni makapi yasiyostahili kuwepo hapo. Mbona vyuo vingine hakuna mambo hayo, wakiambiwa wanakuwa wasikivu lakini hapo naona wanaoingia hapo wengi wanakasoro kunahaja ya kuliangalia hili na kupitia hata records zao za huko wanakotoka, nawashauri katika kutafuta na kufanya huo mchujo msiwaonee aibu TIMUA hata kama wote wataondoka. Sisi ndio tunaolipa Kodi zetu ili wasome siyo kuja Kufanya Madai yasiyoisha. Tunataka tupate wataalamu wasikivu na siyo hawa wanarubuniwa kidogo na Viposha Njaa ili wafanye migomo na kuharibu mali na miundombinu ya Chuo. Chuo Hatua Mliyochukua Ni Sahihi Kabisa.

    ReplyDelete
  8. wanafunzi kwa kweli muwe makini na viongozi wa siasa wenzenu tayari wana vyeti vyao nyie ndio kwanza mnaanza kuyatafuta maisha hamuoni kuwa mnatumiwa sivyo?ndio wazazi wetu wanatuambia tuende vyuoni tujiunge na vyama vya siasa badala ya kusoma?ukweli sisi tunasoma vyuo vya ulaya hatujawahi kuona kuna matawi au wanasiasa kujA vyuoni kuleta uchafu wao inasikitisha kuona ndugu zetu mnavyo hangaika na kutumiwa na wanasiasa inaumiza na haingii ndani ya vichwa kwa nn serikali isipige marufuku vyama hivyo ndani ya vyuo hali hii sasa itaenda mpaka shule za msingi kuanza kuwa na vyama vya siasa ujumbe viongozi wetu wa siasa tunawapenda na kuwa heshim tunawaomba sumu zenu zipelekeni kwa wapiga kura enu majimboni kwenu sio vyuoni wala mashuleni ni nyie haohao kila siku mnalalamika kiwango cha elimu kipo chini kitakuwaje juu nanyi ni vinara wa ushawishi vyuoni?kupoteza muda wao kwa mikutano ya kizushi kwa ajili ya masilai yenu?waacheni wanafunzi wasome

    ReplyDelete
  9. inaonekana wengi wenu wachangiaji humu hamjaenda shule... ni kwanini mshabikie watoto wetu kwenda shule na kupata BORA ELIMU? je kama mlisoma is it fair mwanafaunzi kugraduate bila kuhudhuria mafunzo ya vitendo? je is it fai kuendelea kukiita udom chuo cha kata? TUBADILIKE TUCHUKUE HATUA!!

    SEREKALI ILIPASWA KUWAOMBA WANAFUNZI NA JUMUIYA YA CHUO RADHI KWA KUSABABISHA SINTOFAHAMU, HALAFU NDIO WAENDELEE NA WENGINE,...IT IS HIGH TIME FOR FUKUZA FUKUZA AGENDA... sio mbaya, waende tu hata mahakamani they will get paid LOTS OF MONEY....there is a bunch of graduate lawyers buying cases out here for free!! mtalipwa kama wale wenzenu walivyolipwa..

    ReplyDelete
  10. Sijawahi kuona curiculum review inabadilishwa katikati ya muhula. Kwa wanaotambua ubora wa elimu, inaonyesha Program nyingi UDOM hazijakidhi viwango, na ni vipi TCU iliruhusu zianze kufundishwa kabla hazijakamilika. Bila shaka zitatoa product mbovu maana hazikuwa na learning objectives za course na program zenyewe. Ni vizuri wanaosimamia dhamana ya elimu wasiendeshe vitu kisiasa, Prof. Kikula jaribu kuangalia swala hili kwa undani kabla hatujapoteza fedha na muda wa wanafunzi.

    ReplyDelete
  11. WENGI WENU MNAOCHANGIA HAPA HAMKIELEWI VIZURI CHUO HIKI. ELIMU INAYOTOLEWA HAPA NI YA KIPUMBAVU. KUNA WALIMU WASIO NA QUALIFICATIONS, WANA DIGRII MOJA HAWA NI WENGI SAANA KAMA UKITAKA NJOO COLLEGE OF EDUCATION WAMEJAA TELE. LIBRARY NI KUBWA LAKINI HAINA VITABU, MADARASA YA KUSOMEA YANAVUJA. UKIHOJI TU UNAAMBIWA UNACHOCHEA VUJO CHUONI. HOFU IMETAWALA CHUONI. MANAGEMENT NI WASANII KUANZIA KIKULA NA WENGINE. KOZI AMBAYO MWANAFUNZI ANATAKIWA ASOME MIEZI 4 ANASOMA WIKI 1. KWA UDOM HII NI MAARUFU KAMA EXTREME. MATATIZO KATIKA CHUO CHA UDOM NI MENGI SANA NA UNAPOJADILI NA KUTOA MAONI KUHUSU HILI TATIZO NI MUHIMU KUWA NA FULL INFORMATIONS KUHUSU UDOM VINGINEVYO UTAKUWA UNAWADANGANYA WATANZANIA. UDOM HAKUNA ELIMU BALI NI USANII MTUPU!!!!

    ReplyDelete
  12. KWA KWELI KOSA SI LA WANFUNZI, BALI NI LA SERIKARI KUWADANGANYA WANAFUNZI KUWA WATAENDA FIELD WALIPOGOMA MWEZI WA 12 MWAKA JANA. KUMBE YALIKUWA NI MAJIBU YA KISIASA ZAIDI. NDUGU ZANGU TUACHE TABIA ZA KUWALAUM WANAAFUNZI WANAPODAI HAKI ZAO. VIONGOZI WENGI WA CHUO WANANUFAIKA NA PESA ZA WANAFUNZI. TUWAPO CHUONI TUNAJIFUNZA KUSIMAMIA HAKI, NA CHUONI UKITAKA HAKI KWA NJIA YA MAZUNGUMZO UTAZUNGUSHWA WEEE NA HAKI YAKO HUPATI. NJIA MBADALA NA INAYOKUBALIKA NI HII YA KUANDAMANA. NA KAMA HAMJUI, HII MBINU ILIANZA KARNE YA 19 HUKO UINGEREZA KWENYE KWA WAFAANYAKAZI WA VIWANDA, NA ILIPATA MAFANIKIO.

    ReplyDelete
  13. WACHANGIAJI WENGINE MNACHANGI BILA KUELEWA HALI HALISI YA CHUO HIKI, UKWELI UNAPOTOSHWA KUPITIA VYOMBO VICHACHE VYA HABARI, WANAFUNZI WANAPODAI HAKI ZAO WANAAMBIWA WANAFANYA VURUGU NA KUCHOCHEWA NA WANASIASA JE TUSIDA HAKI ZETU? MFANO COLLEGE OF INFO WALIDAI FEDHA ZA SPECIAL FACULTY WAKAFUKUZWA, SOCIAL WANADAI KWENDA FIELD WAMEFUKUZWA TUSISHANGAE KESHO EDUCATION NAO WAKIFUKUZWA KWA KUDAI FEDHA ZA FIELD. TUJITAHIDI KUJUA UKWELI TUSIPOTOSHWE!

    ReplyDelete
  14. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  15. hawa wanasiasa wa chadema wamegeuza wanachuo kama mtaji wao kisiasa, kwa kuendesha matatizo yasioisha kwani sasa tumewachoka hapa college of education sasa wadai tufanye mgomo pesa ya field ikichelewa

    ReplyDelete
  16. HII NI KWELI BROTHER KWANI HAWA CHADEMA HAPA COLLEGE OF EDUCATON WANATUBOA SANA KILA SIKU WAO NI MATATIZO TU. WANATAKA WAPATIWE HUDUMA KAMA RAIA WA LIBYA KWA NCHI MASKINI KAMA HII. KWAO KILA KITU NI KIBAYA TU.

    ReplyDelete
  17. MCHANGO WANGU MIMI NI KWAMBA WATUACHIE TUSOME NA SI KILA SIKU TUFANYE ISSUE ZA SIASA TU.SIASA ZAO WAZIFANYE NA WANAKIJIJI WA NGONGONA LAKINI SIO KUTULETEA MATATIZO HAPA CHUONI.

    ReplyDelete
  18. HAWA WANAFUNZI WA UDOM WANADAI WALIMU WAO HAWANA SIFA! SIE TUNAWAJUENI ENTRY POINTS ZENU NI DHAIFU. JIULIZENI INGEKUWA BADO TUNA UDSM PEKEE MNGEPATA NAFASI KWENDA UNIVERSITY? NA HIZO DIV. THREE ZENU ZILIZOCHOKA? UWEZO HAMNA MNAJIDAI WAJUAJI.
    ACHANI HIZO.

    ReplyDelete
  19. mtu ambaye ame elimika lazima atajua ubovu wa serikali yetu mafunzo kwa vitendo ndio elimu yenyewe huwezi ukamtunuku shahada mhitimu wa chuo kikuu bila kupitia elimu kwa vitendo wanafunzi wa UDOM endeleeni kugoma mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
  20. Huyo anaesema Entry points za udom ni dhaifu ni mpuuzi! kuna wanafunzi wangap wenye division 1 na 2 udom? au unaandika tu kwa sababu una vidole? ni bora tukawa wachambuzi zaidi ya walopokaji! kama huna taarifa kamili na jambo kaa kimya na sio kulopoka tu, huu ni uwanja wa kujenga na sio kueleza upuuzi wako!

    ReplyDelete
  21. walimu wa udom hawana sifa wala si uongo ni migomo mingapi ya ndani imekuwapo kuhusu walimu hao? kwa uchache kuna walimu wa international relation,na sociology wakiwemo wahindi na mmoja wa watoto wa mkuu wa mkoa hapa nchini? matatizo yapo Udom sema tu hakuna mtu aliyeyaanika na pia uwepo wa wanafunzi wachache wasio wastaarabu ndio kunakwamisha uwazi!

    ReplyDelete
  22. Mgomo wa Udom kuhusu field ni matokeo ya siasa, Mawaziri walipokuwa wanamaliza momo wa mwaka jana december waliahid kuwepo kwa field kwa vitivo ambavyo havikuwa nazo tangu kuanzishwa kwa chuo, ushahidi ni makubaliano ya maandish kat ya uongozi wa chuo, serikali ya wanafunzi na mawaziri wenyewe akiwemo wa elimu na mambo ya ndani, pia prospectus ndogo iliyokuwa na muongozo kuhusu field hizo, na hotuba ya mawaziri hao december mwaka jana vyote hivyo vinapatikana watu wavitafute wajue ukweli, chnzo cha mgomo ni tangazo ambalo lilitoka na kuonesha kwamba hakutakuwa na field tena kwa vitivo hivyo, ni kweli hakuna sehemu ambayo kuna mkusanyiko mkubwa na kukakosekana wahuni, wote hatukubaliani na vitendo vya vurugu katika kudai haki lakini ni bora serikali ikaacha siasa na kuwajibika!

    ReplyDelete
  23. tatizo kubwa la udom ni administration....sasa mgomo wa chuo kizima halafu lawama ziangukie kozi moja? that is real fu**en thinking...mlacha, kikula, kinabo ndiyo ugonjwa pale chuoni..badala ya kuwa BEST university its gonna be the WORST of all in the world kama kutakuwa na danadana zisizo na maana kama hizi za hawa wapuuzi wachache

    ReplyDelete