14 June 2011

Wamiliki 'vipanya' waijia juu SUMATRA

Na Peter Mwenda

WAMILIKI wa daladala zinazobeba abiria chini ya 25 wameipinga Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) kusitisha utoaji leseni ya kusafirisha
abiria katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Bw. Mohamed Masoud Saleh alisema mabasi yao hayatapewa leseni kuanzia Agosti mwaka huu bali yatakayopewa nafasi hiyo ni daladala za abiria kuanzia 35 hadi 60 ndizo zitakazoruhusiwa.

Bw. Mohamed alisema wanajiona watu wanyonge katika nchi yao kwani walihamasishwa kununua Hiace kukabiliana na wingi wa abiria jijini Dar esSalaam lakini sasa wanafukuzwa kama wahalifu.

"Hiace zinapoingia bandarini tunalipa ushuru wa sh. mil. 5 kama gari la biashara, tuliwahi kuambiwa Hiace zetu zisiingie katikati ya Jiji la Dar es Salaam tukakubali na sasa tunakwenda sehemu ambazo hazina miundombinu ya barabara sasa,bado wanataka gari zetu zifutwe barabarani wanataka familia zetu ziishi vipi? alisema Bw.  Salehe.

Alisema wamegundua njama za baadhi ya viongozi wao kukubali mikataba ya kuleta magari makubwa kwa mikopo ambayo yatakopeshwa kwa wenye makampuni lakini wao kama watu binafsi hawatakuwa na faida tena.

"Tunataka Hiace zisifutwe ili kuleta ushindani katika biashara ya kusafirisha abiria jijini Dar es Salaam,hizo kampeni za kununua magari makubwa zitatuathiri sana wafanyabiasha wadogo wa abiria,ndiyo mwisho wetu na familia zetu," alisema Bw. Salehe.

Ofisa Uhusiano wa SUMATRA, Bw. David Mziray alikiri kuwa ofisi yakea ina mapango wa kuondoa aina magari ya  hiace katika kutoa huduma katikakjiji la Dar es Salaama kwania wana kuwa na mradi wa   mabasi makubwa hivyo hazitapata leseni.

"Kama ruti walizokuwa wakifanya kuingia katikati ya jiji zimeondolewa, wabuni njia nyingine za kwenda nje ya Dar es Salaam ambako watapata abiria, kama ni wafanyabiashara wanaotaka kufanya biashara wasome alama za nyakati," alisema Bw. Mziray.

Alisema ubunifu anaosema ni kama ule wa mabasi ya yaendayo Mwenge kutoka Posta ni masafi na madereva na makonda wake ni wasafi wa nguo na utaratibu wa kuhudumia abiria.

Bw. Mziray alisema leseni pia hazitatolewa kwa magari machakavu na kuwataka wamiliki hao kuunda kampuni ambazo zitapewa mamlaka ya kusafirisha abiria kwa mabasi yaendayo kasi.

No comments:

Post a Comment