20 June 2011

Viagra inasababisha uziwi

LOS Angeles, Marekani

MPENDA ngono mkongwe Hugh Hefner, amekuwa na matatizo ya kusikia kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha dawa za kuongeza nguvu ya kufanya
mapenzi Viagra.

Anasema amekuwa akitumia dawa hizo, ili kuwa na nguvu na kuwatosheleza wapenzi wake wakiwemo mapacha wawili wenye umri wa miaka 21.

Mapacha hao wa kizungu, Karrisa na Kristina Shannon wanasema kuwa babu mwenye miaka 85, Hefner hataacha kutumia dawa hizo kwa kuwa hapendi kuacha tabia yake ya kufanya mapenzi.

Karissa alisema: "Alisema ni bora kuendelea kufanya mapenzi kuliko kusikia. Amekuwa na vitu vya kumsaidia kusikia kwa sasa na kwamba anasikia kwa sikio moja tu.

"Unatakiwa kujifunza na kuzungumza katika upande wenye sikio linalosikia ili akuelewe.

"Tunaweza kukaa mbele yake na anaweza kueleza kirahisi kile tunachosema."

Uchunguzi uliofanywa Marekani mwaka jana, ulionya kuwa wanaume wanaotumia dawa za kuongeza hamu ya kufanya mapenzi, Viagra wanakabiliwa na athari za kupoteza uwezo wao wa kusikia.

Daktari wa Sun, Carol Cooper alisema: "Husababisha athari katika neva."

Mapacha wa kike wanaoishi katika nyumba ya Hef mjini Los Angeles kwa miaka miwili, wanasema babu huyo kwa sasa pia amekuwa akipoteza kumbukumbu. Karissa alisema: "amekuwa akisahau hata majina ya mbwa."

Jumanne wiki iliyopita mchumba wa Hefner, Crystal Harris mwenye miaka 25 alitangaza kuachana na babu huyo, akisema hataki penzi la kuchangia na wanawake wengine.

Karissa na Kristina, ambao wameanza kufanya mapenzi na Hef walipokuwa na miaka 18, wanasemekana wanafikiria kurejea katika nyumba yake.

No comments:

Post a Comment