Na Elizabeth Mayemba
TIMU ya soka ya taifa ya wanawake 'Twiga Stars', inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Botswana Julai mwaka huu.Mchezo
huo ni maalumu kwa timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mjini Maputo, Msumbiji kuanzia Septemba mwaka huu.
Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa mmoja wa viongozi wa timu hiyo, ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini kwa madai si msemaji, alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea.
"Tayari Botswana wamethibitisha kucheza mchezo huo, ambao utaisaidia timu yetu kwa ajili ya maandalizi na kutoa nafasi kwa mwalimu kuangalia makosa," alisema kiongozi huyo.
Alisema mchezo huo utaisaidia timu hiyo kujiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo, ambapo Tanzania inapewa nafasi
kubwa ya kufanya vizuri.
Kiongozi huyo alisema tayari Botswana wameshathibitisha kucheza mchezo huo, ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linafanya utaratibu ili mechi hiyo ichezwe.
Twiga Stars imefuzu kucheza fainali hizo bila kucheza mchezo hata mmoja, baada ya Sudan kujitoa katika mashindano hayo.
Timu nyingine zinazowania kucheza fainali hizo ni Nigeria, Ghana, Angola, Afrika Kusini, Zimbabwe, Angola, Liberia,
Zambia, Mali, Guinea, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC, Gabon, Botswana na mwenyeji Msumbiji.
No comments:
Post a Comment