*Asema baadhi zipo kwa mujibu wa katiba
*Mtikila aungana na CHADEMA kuzipinga
Tumaini Makene na Pendo Mtibuche
MJADALA wa kufumua mfumo wa watumishi wa umma na wanasiasa kulipana posho ya vikao umeendelea bungeni katika namna tofauti, ambapo
sasa imetua mezani kwa Waziri Mkuu ambaye pia amerusha mpira huo kwenye katiba, huku pia kukiibuka mipasho ya nani mmiliki wa wazo hilo.
Akijibu maswali ya papo kwa papo jana, Bw. Pinda alisema suala la posho haliepukiki kwani kuna zingine zipo kwa mujibu wa katiba, hivyo haziwezi kuondolewa bila kufuata utaratibu, huku akiongeza kuwa zingine zinaweza kuondolewa kwa maagizo ya Katibu Mkuu akiona inafaa, huku pia akiwarushia kijembe CHADEMA kuwa wapo wanaozimezea mate lakini wanashindwa kusema.
Akijibu swali la Mbunge wa Mkanyangeni, Bw. Mohamed Habib Mnyaa (CUF), Bw. Pinda alisema kuwa ukweli ni kwamba posho hizo ambazo ni stahili za wabunge na watumishi wengine wa umma, zipo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kikatiba na zimegawanyika
katika makundi mawili.
Alisema kuwa suala la posho limewekwa kikatiba na pia katika baadhi ya kazi lipo kwa kulingana na taratibu za kazi yenyewe ikiwemo suala ya fedha kwa ajili ya chakula kwa askari polisi
Alisema makundi mawili ni pamoja na posho ambazo haziwezi kuondolewa hadi kukaa tena kwa bunge na kuziondoa na zile ambazo zinaweza kuondolewa bila kuwepo kwa ulazima wa bunge.
Bw. Mnyaa ambaye alimtaka Waziri Mkuu kueleza suala hilo kwa mujibu wa Katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 73 ambayo inaeleza maslahi ya wabunge wote, wa aina zote, watalipwa posho na mishahara na kifungu cha 26 cha katiba hiyo kinamtaka
kila mtu kufuata katiba.
Swali lililenga kuwa je, serikali inaeleza nini juu ya kadhia inayoendelea kujengeka na wabunge na wanaharakati na kusababisha kuleta fitna kati ya wabunge na wananchi juu ya kupokea posho hizo.
Katika majibu yake Waziri Mkuu alisema kuwa ni kweli stahili za wabunge zipo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kikatiba na wala si dhambi kwa watumishi wengine wa serikali kupata posho na kuwa suala hilo lipo kisheria na kama wabunge wanataka suala hilo liondolewe basi serikali itamwachia jukumu hilo Spika wa Bunge ili
alifikishe kwa rais ili serikali iweze kuona ni hatua gani zitafanyika na baadaye kupelekwa bungeni.
"Kumekuwa na maneno mengi kuwa jambo hili ni kubwa na hata kama mbunge huyo akipewa fedha hizo hazitumii yeye mwenyewe kwani anayo majukumu ya kuwasaidia wananchi na hili ndivyo lilivyo, ni nani atakataa hapa wakati mwingine hujaamka wapo watu nje
ya nyumba yako wanakusubiri uwape nauli na hata wakati mwingine tunashikwa mashati hapa bungeni juu ya kuombwa fedha."
"Jambo hili la kupewa posho ni jambo lililofanyika kwa nia njema katika kuwasaidia wabunge na wananchi wao na serikali inaliona hilo na italiangalia suala hilo kwa wabunge kukataa tu, mi nataka hapa tuwe wakweli kwa upande wetu najua kinachowapata wabunge wengi kwani wapo hata wale wanaoishia kushinda kukopa kwenye mabenki," alisema Bw. Pinda.
Katika swali la nyongeza, Bw. Mnyaa aliitaka serikali kusema kuwa itawachukulia hatua gani wabunge watakaoendelea kukataa posho.
Akijibu swali hilo Bw. Pinda alisema "suala la kukataa posho alianza Kabwe (Zitto) na wengine wa vyama vingine wakaunga mkono lakini sisi tunasema kuwa ni jambo jema kwani wapo waliowahi kujitoa na hata kutoa mishahara yao kwa kipindi cha nyuma
kusaidia wananchi...lakini hata hivyo ndani ya CHADEMA wapo baadhi ya wabunge ambao wanazimezea mate posho hizo, japo hawawezi kusema.
"Unaweza ukasema posho yangu nisipewe ukataka ibaki hazina na ipelekwe sehemu fulani, it is fine, there is no problem. Ninachoogopa kusema ni kulifanya jambo hili kuwa kubwa," alisema Bw. Pinda na kuongeza.
"Inajulikana kwamba, stahili wa mbunge zipo kwa mujibu wa Katiba au taratibu zilizopo, vile vile niseme tu kwamba, zipo posho za aina mbili, zipo ambazo Katibu Mkuu hawezi kuzirekebisha kwa sababu zipo kwa mujibu wa sheria na zingine ni zile ambazo Katibu Mkuu anaweza kuzirekebisha kulingana na jinsi anavyoona inafaa.
"Ambazo katibu mkuu hawezi kuzirekebisha ni kama zile wanazolipwa madiwani, madiwani hawana mishahara, posho wanazolipwa ndizo zinazowasaidia kutimiza majukumu yao, askari wao wana kitu kinaitwa 'ration allowance' sasa hizi huwezi kuziondoa.
"Wapo wafanyakazi wanakaa katika vikao hadi usiku, hawa wanalipwa posho kama motisha ya kazi wanazofanya, wapo wengine hasa hawa wanaoandaa bajeti, wanakaa kwa muda mrefu katika vikao, hawa ukiwalipa posho siyo dhambi, wanalipwa kama njia ya kuwa
'motivate' tu.
"Sasa hizi za wabunge, Spika anaomba kibali kwa Rais, nalo sasa naona limekuwa jambo kubwa, tuelewe kwamba sehemu kubwa ya posho wanazolipwa wabunge ndiyo hizo hizo wanazowapa wananchi, kwa mfano unaweza kuwa uko hapa ndani, pale mlangoni kuna
mtu anakusubiri, ukitoka nje tu anakuomba fedha, unaweka mkono mfukoni unampatia.
"Watanzania wasilione jambo la ajabu, walione jambo la kawaida lakini kwa kuwa serikali imeshaliona, italifanyia kazi," alisema Bw. Pinda.
Tangu Jumanne iliyopita kumeibuka hoja juu ya nani 'mmiliki' wa hoja hiyo ya kufumua na kuondoa mfumo wa posho za vikao, ambazo baadhi ya wachambuzi wanasema ni sehemu ya tatizo la matumizi makubwa ya serikali yasiyokuwa na tija, ambalo linachukua takribani zaidi ya sh. bilioni 900 kwa mwaka.
Hoja hiyo ilianzishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ikiwa ni moja ya mapendekezo yake ya kupunguza matumizi makubwa ya serikali yasiyokuwa na tija, badala yake ikitaka fedha hizo zielekezwe katika miradi ya maendeleo ya wananchi.
Tangu kuanza kwa hoja hiyo takribani wiki tatu zilizopita, kwenye vikao vya kamati za kudumu za bunge, Dar es Salaam, baadhi ya wabunge, hasa wa CCM na mawaziri, walisikika wakipinga wakisema ni suala ambalo haliwezekani, kwani liko kwa mujibu wa sheria na taratibu ambazo wamezikuta na hawawezi kuziacha.
Lakini Jumanne baadhi ya wabunge waliibuka na hoja kuwa suala hilo si geni, wala CHADEMA wasijifanye kuwa ni la kwao, bali tayari serikali imeshaliona na kulipendekeza katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16), hivyo hoja ikabadilika kuwa 'CHADEMA wameiba' wazo hilo.
Hoja hiyo imekuwa ikichukua taswira tofauti ndani ya ukumbi na nje katika viwanja vya bunge, pia katika jamii, ambapo wakati mwingine wengine wamejikuta wakijadili watu zaidi, badala ya hoja yenyewe.
Kauli ya Mtikila
Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amesema anaunga mkono CHADEMA kwa asilimia 100 kupinga posho za vikao wanazolipwa wabunge na watumishi wengine wa serikali kwa kuwa ni sehemu ya majukumu ya kazi zao.
Pia Mchungaji Mtikila ameisifu bajeti ya kambi ya upinzani iliyosomwa bungeni juzi na Waziri Kivuli wa Fedha, Bw. Zitto Kabwe, kuwa ina sura ya huruma, ukombozi na kujali Watanzania wanaoishi maisha ya chini kabisa.
Mchungaji Mtikila alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kufungua kesi nne katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu dhidi ya Serikali ya Tanzania.
"Nimesikitishwa na kiwango kikubwa cha fedha kilichotamkwa na CHADEMA kutumika kuwalipa posho wabunge huku Watanzania waliowachagua hawana uhakika wa kula, mimi kwa hili naungana na CHADEMA kupinga vikali.
"Kama suala hilo litashindwa kuamuliwa bungeni au kubadilisha hiyo sheria wanayodai ni halali kulipwa, ni vema likawahishwa mahakamani," alisema Mchungaji Mtikila.
mh, mbona pinda haeleweki, hapo what matters ni wabunge!!!!! mambo ya madiwani mbona tunayafahamu, i think anajaribu kulifanya dogo ili wananchi tusisimke pale tunapoibiwa
ReplyDeleteUMETUFUMBUA MACHO MHESHIMIWA KUMBE WANAPEWA ILI WATUSAIDIE SHIDA NDOGO NDOGO? SASA UMETUFUMBUA MACHO KWA KWELI. TUTAENDA KUWAONA WATUSAIDIE NASI TUPATE UNAFUU.
ReplyDeleteSASA NI BORA ATENGENEZE MAZINGIRA BORA JIMBONI ILI ASISUMBULIWE NA OMBA OMBA AOMBAO NI KERO AU NI BORA AGAWE HELA KWA MTU MMOJA MMOJA? JE! AMBAYE HANA HABARI HII YA KWENDA KUOMBA HELA KWA MBUNGE WAKE INAKUWAJE? KWA STAILI HII TUTAFIKA? TUBADILIKE JAMANI TUSIJIANGALIE WENYEWE. SIKU ZOTE MWANZO MGUMU.
CHDMA WANAWADANGANYA WA TZ KILA SIKU AFADHALI WAMEJICHANGANYA NA KUTAKA KUKIUKA KATIBA YA NCHI , NA KUJIDAI WANAHURUMA YA KINAFKI , KIKUBWA NI KUPATA KATIBA MPYA YA KUONDOA POSHO NA SI KUDANGANYA WATU KWA KUVUNJA KATIBA YA SASA ILI HALI WAMEAPA KWA MUJIBU WA IBARA YA 73
ReplyDeletechadema wamefilisika , ahsante Mnyaa wa CUF KWA kutufunua macho kuwa udikteta wa CHADEMA wanataka kuuhamishia kwenye kudhalilisha katiba ya nchi , waliyoapa kuitetea, washindwe na walegee.
ReplyDeleteMaskini CHADEMA udikteta wenu umeumbuka., mmeapa kuteteaKATIBA YA NCHI ya mawazo yenu? HONGERA CUF KWA MUENDELEZO WENU WA UKOMBOZI WA KWELI NA SI UNAFIKI, KAMA HAWATAKI UBUNGE WABUNGE WA CHADEMA WAJIUZULU
ReplyDeleteTunaipenda TZ na tunapenda mawazo ya kujenga si unafiki CHADEMA mmechemka, Zitto ashauri kwanza Mbowe anyanganywe gari la serikali na posho ya milioni mia moja (100,000,000?/=) Tsh. ya kuendeshea kambi ya upinzani kwa mwaka , CUF msizubae wakomboeniw wa Tanganyika maana wamedanyangwa hadi miaka 50 ya uhuru
ReplyDeleteCHADEMA , ZIIIIIII! ahadi zenu majimboni mmetekeleza au mmeAMBIWA MBUNGE NI SEHEMU YA KUVUNJA KATIBA?
ReplyDeletetuwazomee hao CHADEMA ooooooo! sifa za kijinga mwisho, kama wanataka waanze na kumnyanganya Padri Slaa posho ya ml.7 ambayo ni jasho la wa tz
ReplyDeleteAHADI ZAO VIPI? CHADEMA KIFUTWE
ReplyDeleteHuyu Jamaa vipia anazeeka vibaya ama eshalewa uccm? Yaani kwa akili zake anaona wananchi kusaidiwa hela ni vyema zipitie kwa wabunge kisha zichujwe na kutiririka kwa walala hoi waliowapeleka bungeni? Na je, hizo posho za watumishi wa serikali nazo wanawagawia walala hoi? Viongozi wa ccm wasanii wakubwa.
ReplyDeleteHawa jamaa hawakuyasikia aliyoyaeleza Rais wa zamani wa ujerumani. Viongozi wa ccm wamezamisha vichwa mchangani, hawasikii wanavyobezwa na kudharauliwa na wale wenye kutoa misaada. Bure kabisa
cuf kumbe mnajua kujibu hoja? mbona hamjafanya maandamano turudishe kadi za chadema na ccm?
ReplyDeleteJamani sisi watoa maoni tutumie busara si kuandika tu upupu ili mradi. Kama mtu hana hoja ya maana akae tu kimya. Hizi posho na ziondolewe kabisa kwani watanznaia wote si waajiriwa. Hizi posho zinawanufaisha wachache sana kwa sababu zinalenga wabunge, viongozi na watumishi wenye ajira serikalini tu! Sasa wakulima, wafanyabiasha wananufaika nini? Wote mjue ni watanzania na hizo posho ni kodi zetu sote. Mimi nionavyo mtu akilipwa mshahara unatosha posho zifutwe. Hongera sana Zitto kabwe kwa kuibua huu mjadala angalau umeonyesha uzalendo si sawa na kina Cheyo wa UDP ambaye ameshazeeka hajui tena la kufanya yeye bado anadai kuwa wala posho hazitoshi ziongezwe.
ReplyDeleteBaada ya kujivua gamba sasa tumeweza kuiona rangi halisi ya nyoka,CCM muanze kupaki, 2015 sio yenu.Ni vyema mkasoma harama za nyakati mapema,the writing is on the wall- YOUR TIME IS OVER.
ReplyDeleteNimeamini Busara si Umri, Pinda unajibu kama Bambo wa the comedy.Aibu kuwa na PM kama wewe
ReplyDeleteCHADEMA CHALI, POSHO HAZIEZI KUVUNJA KATIBA YA NCHI , MNGEPEWA NCHI MNGEKUWA MADIKTETA , MMEAPA KUTETEA KATIBA YA WAPI? NA WATANZANIA MNAOSUBIRIA CHADEMA KUFIKIRIA NDO WAWAELEZE MBADILIKE ,
ReplyDeleteHuyu mzenji Mnyaa anatia ki nyaa! Ni njaa zao tu, wanakula bara na pwani! Kwani wanauchungu gani na hela zinatoka hazina bara? Hawa ndio wanauza magari kabla hayatoka show room! Kwani zenji wahitaji shangingi VX la nini? Wachumia tumbo hao siku muungano ukivunjika watalia na kusaga meno. Kwani si unasikia kauli za Rashid? Anasema posho si jambo la msingi kuongelea!
ReplyDeleteJamaniee tusidanganyike,ni wananchi wangapi wanasaidiwa nao wabunge,wakati wabunge wenyewe huyakimbia majimbo yao mara tu baada ya kupewa kula?kuhusu kwamba eti ni suala la kikatiba hili pia halina
ReplyDeletemshiko,mangapi yapo kwenye katiba wameyapiga buti hili ndo waliona la muhimu,pia katiba sio msaafu thus why tupo kwenye mchakato wa rasimu ya kuundwa nyingine,suala hilo linaweza kuondoshwa tu
UJINGA WENU WATANZANIA HIVI HAO WASIOZITAKA HIZO POSHO SI WACHUKUE WENYEWE WAPELEKE MAJIMBONI MWAO AU KWENYE VYAMA VYAO,MNATANGAZA ILI IWE VIPI? MBONA HAWATUAMBII WAMEISHA PELEKA NGAPI HUKO MAJIMBONI MWAO? WAPO WABUNGE WAFALME KUTOKA UPINZANI HUMO NDANI SASA ZIPO DALILI ZA HUKO MAJIMBONI MWAO KUCHOKWA MAANA WAMEISHAKAA MUDA MREFU KAMA AKINA MALECELA WA CCM SASA HOMA INAWAANZA MAPEMA KWA HOFU YA KUCHAGULIWA TENA MAJIMBONI MWAO NDIO WANAANZA VITUKO. CHUKUA POSHO YAKO PELEKA JIMBONI KWAKO UNATAKA SERIKALI IKUPELEKEE BAADAYE UWADANGANYE WAPIGA KURA WAKO KUWA ULITOA MAPESA MENGI LAKINI HAYAJALETWA JIMBOMBONI BEBA MSALABA WAKO MWENYEWE KWA KUPELEKA POHO YAKO JIMBONI KWAKO. TUACHE SIASA ZA SOKONI HATUNA UMEME MNATULETEA MASUALA YA KIJNGA KAMA HAYA NA VIJIBWA VYENU VINASHANGILIA
ReplyDeleteKweli Tanzania mambo bado ni magumu sana.Hapa naona kunawatu wanatoa maoni kana kwamba wanataka hizi posho ziendelee.Kweli sasa nimeamini kuwa bado tunatatizo kubwa sana la uongozi.Hata waziri mkuu badala ya kutetea wananchi yeye anasema posho(ulaji) hauepukiki kweli kazi ipo.Sasa hivi mnagombania posho wakati kule longodo watu wanakufa njaa hawanachakula.kama posho haziepukiki kwa sababu ya katiba hii haina maana kwa sababu katiba imetungwa na watu na watu haohao ndio watakaoirekebisha hiyo katiba.Hili suala la kusema kuwa posho haiepukiki maana yake ni nini?Yaani kila siku nyie mlio madarakani muendelee kuponda raha na maisha mazuri wakati wananchi waliowaweka madarakani wanaishi maisha ya ufukara.Sawa kuna siku hizo posho zitawatokea puani.
ReplyDeletePinda ameanza kutoa makucha yake halisi, anakuwa kama mzee wa vijisenti kwani analiona hili la posho ni jambo dogo sana badala ya kujadili mambo makubwa, je mambo makubwa niyapi? Halafu wachangiaji hapo juu hakika sioni huruma yenu hata kidogo huenda ni ushabiki usio na msingi hivyo waalimu, wauguzi posho zinatoka wapi?
ReplyDeleteCDM NI WASANII KAMA WA BONGO FLEVA MAANA HUWA WANAKURUPUKA TU NA HOJA ILI KUPATA UMAARUFU. HII INAONYESHA HATA HIYO KATIBA HAWAIJUI, WANGETUAMBIA TUPIGANIE KUBADILI HICHO KIFUNGU CHA KATIBA KATIKA KATIBA MPYA KUSIWE NA POSHO HIZO TUNGEWAONA WA MAANA.LAKINI WAO WANAFOSI ZIFUTWE KIENYEJI KISHA WAJE WAZIDAI BAADAE KWA KUWA ZIKO KWA MUJIBU WA KATIBA.
ReplyDeletechadema chali , kifo cha mende , wajifunze kwa Kenya , wanaheshimu katiba ya nchi na hata uteuzi ulopendekezwa wa majaji wa mahakama kuu ya rufani (suppreme court) umesimamishwa hautafanyika Jumatatu , tunawashangaa watanzania CHAMA TUNACHOONA KITAWAUNGANISHA HUKO TZ HAIEZI KUWA CHADEMA , CHADEMA WANAPENDA KUSIFIWA TU, NI DICTATORIAL PARTY , NA HAO CUF WAELEWESHENI KUWA KAMA HAWATAKI KUWAUNGANISHA ICHI WAFUTWE MAANA CCM IMESINDWA KWA MIAKA 50 YA UHURU
ReplyDeleteAhsante mkenya kuchangia, CHADEMA imezeeka, waliapa kulinda katiba ipi? katiba inabadilishwa kwa barua? hawafai
ReplyDeletewaalim na madaktari mbona hawana posho?mtadaije posho kwa kazi yenu wakati mnalipwa mishahara.waoneeni huruma walala hoi na wale wote waliowapa kura kwa manufaa ya maendeleo.
ReplyDeleteWAZIRI hili sio swala dogo kama unavyolifikiria,wananchi tunakosa imani na wewe.huwezi kusema hili ni swala dogo kua wabunge wanalikuuza.mheshimiwa toa maamuzi yenye tija kwa wananchi pamoja na nchi kama ulivyowahi kuongelea swala la mauaji ya walemavu wa ngozi bungeni mbona tulikuelewa
ReplyDeletewaziri ule uchungu ulioutoa juu ya mauaji ya walemavu wa ngozi umeupotezea wapi?leo unasema kua suala la posho ni dogo wabunge wanalikuza!tunapoteza imani na wewe mheshimiwa!
ReplyDeleteBunge la Tanzania ni bunge la masilahi yao binafsi na wala siyo bunge la kutetea mwananchi ambaye kipato chake kwa siku ni chini ya dola moja,hakuna siku na moja mtanzania wa hali chini atasema anambunge wa kutetea hoja zake au shida,tofauti na wao wabunge kujilimbikizia wingi wa posho na kwa ajili masilahi yao binafsi.
ReplyDeleteWATANZANIA TUJIFUNZE JINSI YA KUJENGA HOJA NA KUACHA KULALIA UPANDE MMOJA PANAPOKUWA NA SWALA LA KUJADILI JUU YA MAMBO YANAYOENDELEA NCHINI KWETU. TUACHE MATUSI NA JAZBA NA TUHESHIMU KILA KAULI YA MMOJA WETU KULINGANA NA MAONI YAKE. AU LA NINI MAANA YA KUJADILI HUMU?
ReplyDeleteMIZE PIND..A...NI MSANII, ALIJIFANYA KUTOA MACHOZI SWALA LA ALBINO, AKAJIITA MTOTO WA MKULIMA KUMBE HANA DHAMIRA YA DHATI, ANATETEA POSHO ZA WABUNGE KWA HOJA DHAIFU KUWA POSHO ZINATUMIKA KUWAGAWIA WATU WANAOOMBAOMBA KWELI PINDA KWELI PINDA MTOTO WA MKULIMA UNASEMA HAYO???!!!!!
ReplyDeleteKWELI NI HAKIKA NDANI YA SISIMAJAMBAZI HAKUNA ALIYE SAFI.
UKISHAKUA MWANASIASA BASI WEWE UJUE MOTO UNAKUHUSU,KWA KWELI HAWA VIONGOZI WETU WANAJIPENDELEA SANA TENA SANA NA WALA HAWAFIKILII KABISA WANANCHI WA HALI YA CHINI INAUMA SANA NA HUYO KIONGOZI UKIMTOA HAPO KWENYE UONGOZI ALIE NAO KWA GHAFLA BASI ANAWEZA KUFA MAANA MAPESA ANAYOPEWA NI MENGI MPAKA WANAKUWA WANAFANYA KUFULU LAZIMA KWA KILA NJIA YAPUNGUZWE HAYO MAESABU YAO WEWE MPAKA SCHOOL ZA SERIKALI MADAWATI TUNASUBIRI MSAADA WA MASHIRIKA AU TAASISI ZA WATU BINAFSI INAMAANA HAWAONI AIBU HATA KIDOGO HII LEO WANAFUNZI WANASOMA WANAKAA KWENYE VUMBI,HOSPITAL WAGONJWA WANALALA CHINI,N.K TAFADHALINI WAHESHIMIWA KWELI MUONE AIBU MAMBO MENGINE NA PIA MNATUTUKANISHA SISI TULIOPO NNJE YA TANZANIA TAIFA TAJIRI NNCHI IMEOZA KILA KATIKA KONA,TUMIENI JINA LENU LA WAHESHIMIWA MUONEKANE KWELI WAHESHIMIWA SIO KIINI MACHO,MUNGU IBARIKI TANZANIA KWA KILA AINA YA MAENDELEO YA DUNIA YA HIVI SASA NA HUKO TUNAKOELEKEA KWA VIZAZI VYETU VYA BAADAE.
ReplyDeleteUshauri mdogo kwa CHADEMA Serikali ni ya CCM nyie toeni ushauri ,maoni yenu Yatosha. Posho hizi chukueni kwa sababu serikali ni ya CCM mtu hakitaka kuaribu kitu chake msaidie kuaharibu.Chukueni hizo posho mkae kama Chadema na pesa hizo za posho mkafanyie maendeleo sehemu nyingi zinaitaji maendeleo
ReplyDelete