Na Stella Aron
KIKOSI cha Kupambana na madawa ya kulevya nchini kimewatia mbaroni baadhi ya viongozi wa dini na mabalozi kwa na dawa ya kulevya.Mkuu wa Kitengo cha
Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Bw. Godfrey Nzowa alisema katika kipindi cha mwaka 2009/ 2011 baadhi ya viongozi wa dini na mabalozi na wafanyabiashara wengine wakubwa wa dawa hizo kutoka nchini na nchi za nje wamekamatwa.
Kwa mwaka 2009 kikosi kiliwakamata wasafarishaji watano wa Heroin wakiwamo baadhi ya viongozi wa dini na mabalozi kwa kukutwaa na kilo 9, wawili Cocain wakiwa na kilo 4, na kuteketeza ekari 79 za mashamba ya bangi na kuwakamata watumiwa tisa.
Mwaka 2010 kikosi hicho kiliwakamata washtakiwa 496 wa Heroin ambapo wasafirishaji 10, watumiaji 480 na wafanyabiashara sita ambapo wanne walitoka Iran na wawili walitoka Afrika Kusini.
Alisema ekari 296 ziliteketezwa na watuhumiwa wanne walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
Bw. Nzowa alisema mwaka jana kikosi hicho kiliwakamata wafanyabiashara wakubwa kutoka Pakistan, Nigeria, Kenya ambao wengine walidai kuwa wanakuja nchini kwa ajili ya kanisa na wengine ni mabalozi.
"Ukiwaona jinsi walivyovaa na mizigo yao hutoweza kufikiria kuwa kwenye mabegi wameficha dawa za kulevya kutokana na jinsi walivyofunga," alisema.
Alisema Machi 3, mwaka huu kikosi hicho kilimkamata mtuhumiwa mmoja kutoka Nigeria ambaye alidai kuwa amekuja nchini kwa ajili ya huduma ya kanisa lakini haikuwa hivyo.
Alisema kuwa kundi lingine ni wafanyabiashara maarufu kutoka nchi za jirani ambao waliingia nchini kwa kivuli cha mabalozi wa nchi mbalimbali huku wakiwa na sifa za mabalozi husika na katika uchunguzi ikagundulika ni wauzaji wa dawa za kulevya.
"Kila mtu anaingia nchini kwa vigezo vyake na tunapofanya uchunguzi tunabaini kuwa ni wauzaji wa dawa lakini walitumia njia ya udanganyifu kuingia nchini," alisema.
Hata hivyo alisema kuwa katika kupamba na uuzaji na usafirishaji wa dawa hizo, Juni Mosi mwaka huu kikosi hicho kilimtia mbaroni mfanyabiashara maarufu mwanamke anayeonekana kwa sura sita.
Mtuhumiwa huyo anayefahamika kwa majina mengi kama Mwanaidi Mfundo au Nahima Mohamed au mama Leila alikamatwa saa 8 usiku, Mbezi Beach, Dar es Salaam akiwa na kilo tano za Cocain na lita tatu za Chloroform.
Pia mtuhumiwa huyo alikamatwa na watuhimiwa wengine ambao ni Bw. Antony Karanja Arthur (Mkenya), Bw. Ben Machania (Kenya), Bi. Saraha Munuo (Mtanzania), Almas Saidi (Mtanzania), Bw. Yahaya Haroun (Mtanzania) na Bi. Aisha Kungwi (Mtanzania). Wote wamefikishwa mahakamani.
Please Mr Nzowa,uwa nafuatilai sana taarifa za wanokamatwa na dawa za kulevya,sijawahi kusikia ukitaja viongozi wa dini,sasa suala liliopo sasa ni tamko la mheshimiwa raisi ,tuanomba kama ulivyowataja kwa majina awa washitakiwa uliokamata juzi tunaomba pia ututajie kwa majina viongozi wa dini uliokamata,walikamatwa lini ,ni voingozi wa dini gani na wananydhifa gani etc.Please tuondolee huu utata na tuendelee kulinda heshima ya raisi wetu.Pia wewe ulituhumiwa na Mengi,je iliishhia vipi,tulisikia umehamishiwa makao makuu,mbona unaendelea kuwa msemaji wa kikosi cha madawa ya kulevya?
ReplyDeleteMi binafsi napenda kumpongeza kamanda nzoa kutimiza majukumu haya ktk mazingira magumu ya watu wagumu na wajanja mithili ya mpanya mungu akubariki na usKIWANJAkalinga hili kwani hali ni mbaya sana
ReplyDelete