13 June 2011

Mwenyekiti CCM avuliwa uanachama

Na Moses Mabula,Tabora

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tabora kimemvua uanachama wa chama hicho Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Gongani, Bi. Rajia Mrisho huku kikimwondoa
Bw. Emmanuel Kasoga katika nafasi ya Katibu Kata CCM, Kata ya Bukumbi wilayani Uyui.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Tabora Bw. Hasasn Wakasuvi alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na utovu wa nidhamu uliooneshwa na makada hao.

Alisema kuwa hatua hiyo ilifikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa baada ya kubaini ukiukwaji wa maadili ya chama wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana.

Alisema kuwa chama hicho kamwe hakitaona haya kumwajibisha mwanachama ambaye atakiuka taratibu na kanuni za chama kama zilivyoainishwa kwenye katiba yake.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo hakuweza
“Ndugu zangu wanahabari mengine haya ni siri ya chama kwa hiyo siwezi kuwaeleza zaidi nini hasa kimesababisha watu hawa kuchukuliwa hatua hizi," alisema.

Hata hivyo habari za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zinasema kwamba viongozi hao walikihujumu chama wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

2 comments:

  1. Sawa lakini mkumbuke pia tunataka maendeleo mkowa wetu umesahaulika ni bora hata kabla ya uhuru tabora ilikuwa na umaarufu kwa kila fani leo hii unashindwa kuilezea tabora viongozi wabaguzi maana haiwezekani mikowa ya magharibi tu iwe katika hali hii na nyinyi mliopata hiyo nafasi siyo mpoteze muda wote na siasa wakati maendeleo hakuna tumechoka.

    ReplyDelete
  2. Haya endeleeni kuvua magamba, mwisho wake kutakuwa hakuna chama cha magamba. Hao wanaovua wenzao magamba, wao sio magamba?

    ReplyDelete