*Yamsimika askofu aliyezuiwa Arusha
Na Mwandishi Wetu Arusha
PAMOJA na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kusitisha kusimikwa kwa Askofu Mteule wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Mchungaji
Stanley Hotay, kiongozi huyo amesimikwa kama Askofu wa Kanisa la Anglikana.
Waumini wa dayosisi hiyo walipinga kusimikwa kwake mahakamani kwa kufungua kesi mbili moja ya madai namba 18 na nyingine ya jinai namba 48 wakiiomba kuzuia sherehe za kusimikwa kwake kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kugushi umri wake, lakini wamegonga mwamba.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Arusha jana, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini, Dkt. Valentino Mokiwa alisema wamemsimika kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania na si Askofu wa Dayosisi hiyo ya Mount Kilimanjaro inayopiganiwa mahakamani.
Alisema Mahakama hiyo imezuia Mchungaji huyo kusimikwa Uaskofu wa Dayosisi hiyo na si kuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, na iwapo shauri lililopo mahakamani litamalizika vizuri, Askofu huyo atatawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo.
Waumini waliofungua kesi hiyo ni Bw. Lothi Oilevo, Bw. Godfrey Mhone na Bw. Frank Jacob wanaotoka Parishi ya Mtakatifu James, Dayosisi hiyo ambayo pia ilielezwa ni wajumbe wa Baraza la Walei.
Hata hivyo hafla hiyo iliyofanyika bila shamrashamra kubwa, ikiwa imehudhuriwa na waumini wachache wakionekana kukosa amani kutokana na amri ya mahakama huku kukiwa na ulinzi mkali wa askari kanzu na wanausalama wakipita huku na kule kuangalia usalama.
Akitoa uamuzi huo Ijumaa iliyopita, Jaji Kakusuro Sambo alisema baada ya kusikiliza maombi ya walalamikaji kutaka shauri hilo lisikilizwe kwa dharura na hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, kesi hiyo iliahirishwa kwa lengo la kutoa uamuzi wake leo huku ikitoa amri ya kutofanyika chochote.
Hata hivyo, wakati Mahakama Kuu ikizuia Askofu huyo kusimikwa, tayari wageni mbalimbali wakiwemo maaskofu na viongozi wa kanisa hilo wa ndani na nje ya nchi, walikuwa wamewasili Arusha kwa ajili ya ibada hiyo.
He! huu si uhuni? Kanisa hili vipi? Sasa tuone kama mahakama itaamuru wakamatwe? hakuna chenga yoyote hapo hao wamekiuka zuio la mahakama.
ReplyDeleteAcheni wivu ninyi mlioweka pingamizi la kihuni. Hamtashindana na wakuu hata siku moja. mtabaki hivyohivyo.
ReplyDeleteJamani tuseme ule ukweli, askofu mkuu anakubali kumwema mtu anayetuhumiwa na tatizo la jinai! Yaani amegushi umri hilo ni kosa kubwa la kimaadili sawa na mtu akionekana mlevi au amefumaniwa hivi kweli atawekwa mikono kuwa mchungaji achilia mbali kuwa askofu. Tena tunasikia askofu Makundi aliyemweka mikono ya uchungaji huyu bwana hakuhudhuria. Na yeye anajua wakati kumweka mikono ya ushemasi umri aliousema inakuwaje sasa askofu mkuu asimsikilize mtu aliyemweka mikono na ushahidi upo wazi jamani. Askofu Makundi anajua wazi kwamba huyu bwana amefoji umri ili tu awe askofu! Jamani kanisa tunalipeleka wapi? Huyu hastahili hata kuwa mchungaji kwani ni mwongo ana weza kufanya hata biashara ya madawa ya kulevya. Sasa hivi mahakama ikirithika kwamba kweli alifoji umri ndo mtamwoondolea uaskofu kwa sababu atakuwa na kosa la kimadili. Hapa siyo kuvunja katiba lakini ni kufoji ambalo ni kosa la jinai.
ReplyDeleteIkija tokea mahali pengine hapo ndo mtakuja kusema hapana? Katiba kazi yake nini? sasa hapo? Askofu mkuu kafanya uhuni mkubwa sana. Huyu askofu mkuu amekuwa anasababisha mizozo mingi sana kwenye kanisa Anglican Tanzania. Hafai kabisa kuwa askofu Mkuu. Kwanza hana busara kabisa. Angalia anavyoropoka kwenye vyombo vya habari akiituhumu serikali wakati yeye mwenyewe ni fisadi wa kutupwa. Jamani waanglican tuondoleeni huyu mtu. Ushirikina ndio umemweka hapo tu. Na si sifa ya utendaji kazi ulitukuka. Tunachoomba mahakama iamue kwa haki juu ya jambo hili.
Askofu Mkuu Mokiwa analiangusha kanisa la Anglikana. Toka awe askofu Mkuu amekuwa mtetezi wa mapdre ambao ni wahuni, walevi ,fuska,na wezi ni kanisa gani ambalo halina miongozo ya kuchagua watendaji wake? kanisa hili linakwenda wapi? kiongozi huyu hafai kwa sababu ndio kiongozi wa mabaya yote hayo, askofu ni mchkuwaji wake za watu , wasichana wadogo, na hukutana nao nje ya nchi kwa fedha za sadaka toka kwa waumini. Atatoaje masaa 48 kwa Rais wa Nchi au yeye ndie mtoa hati za wauza unga na anaogopa kuumbuliwa? Askofu vua gamba au waumini watakuvua hivi karibuni, na kama hutataka kuondoka ujue utaongoza kanisa hilo bila waumini maana wengi sasa wanahamia makanisa mengine utajikuta uko peke yako na wachungaji mafuska na wezi.waachie wenye roho safi na wenye wito wa kuongoza kanisa wewe huna wito huo.
ReplyDelete