Na Grace Ndossa
KIONGOZI wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe, (CHADEMA) amekiri kutokujaza fomu za kutaja mali zake kama inavyotakiwa na Tume ya Maadili ya Viongozi wa
Umma kutokana na msongo wa mawazo.
Ametaja sababu ya msongo wa mawazo yaliyomfikisha katika hatua hiyo kuwa ni masuala ya kisiasa zikiwemo kesi katika maeneo tofauti nchini.
Akijitetea mbele ya Baraza la Maadili ya Tume hiyo Dar es Salaam jana, chini ya Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Damiani Lubuva, Bw. Mbowe alisema amechanganyikiwa kutokana na kesi hizo hivyo kushindwa kujaza fomu hizo.
Alisema tangu aingie madarakani amepata misukosuko mingi zikiwemo kesi katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha, Mahakama ya Moshi na Mahakama ya Hai, hivyo alichanganyikiwa kutokana na kesi hizo.
"Nakiri kutojaza fomu hizo za kutaja mali zangu kwa wakati kutokana na usongo wa mawazo uliotokana na masuala ya kisiasa zikiwemo kesi katika maeneo tofauti nchini," alisema Bw. Mbowe
Alisema ilikuwa vigumu kwake kujaza fomu hizo kwa wakati akihofia kuandika vitu visivyo sahihi kutokana na kuwa na makazi katika sehemu tofauti ikiwemo Dar es Salaam, Kilimanjaro na Dodoma.
"Nimekuwa nikisafiri mara kwa mara, naomba baraza lako liniwie radhi kwa kuchelewa kujaza fomu hizo kwa wakati uliotakiwa," alisema Bw. Mbowe.
Aisema barua ilitumwa katika ofisi yake ya Dar es Salaam wiki mbili huku vikao vya bunge vikiwa vinaendelea na fomu alijaza Mei 30, mwaka huu na kuziwasilisha juzi akiwa ameshapata barua ya wito.
Mahojiano kati ya Bw. Mbowe na na Jaji lubuva ilikuwa hivi;
Jaji Lubuva: Ni kweli mheshiwa mbunge ulikuwa na majukumu mazito hukuona kwamba ni busara kutenga muda, kuanzia ulipoapishwa ulishindwa kabisa kupata muda? Na kama ni hivyo ulishindwa kabisa kutoa taarifa kwa wanaohusika?
Bw. Mbowe: Mheshiwa Jaji msongo wa mawazo una matatizo mengi kama nilivyojieleza katika utetezi wangu wa awali, mheshimiwa naomba radhi tu kwa hili.
Jaji Lubuva: Ni kweli nimepita katika matatizo mengi lakini wewe kama ulivyosema wewe ni kiongozi wa kitaifa inakuwaje katika mambo yako yote ukashindwa hata kukumbuka kutoa taarifa?
Bw. Mbowe: Nashukuru mheshimiwa jaji, labda nisome hii barua ya tarehe 14/1/2011, barua hiyo ilisainiwa na E. Mrema Kaimu Katibu wa bunge.
Kama nilivyosema awali barua hii nilipokea mwezi wa tano wakati Kamati za Bunge zikiendelea sisi viongozi tunatofautiana kwa mazingira, maeneo tunayokaa, mazingira ya kazi niliyonayo nitashindwa kujaza fomu kwa usahihi na nilihofu kuandika taarifa za uongo, naomba radhi sikufanya kwa makusudi.
Mwanasheria wa Sekretarieti Tume ya Maadili, Bi. Getrude Cynacus: umeeleza msongo wa mawazo ndio umekufanya ushindwe kujaza fomu na mambo mengine umeisoma ile fomu?
Mbowe: Ndiyo.
Mwanasheria: Unafikiri wale wote waliopo mle bungeni hawana msongo wa mawazo?
Bw. Mbowe: Siwezi kuwasemea wao wana majukumu gani.
Mwanasheria: Unafikiri sababu hiyo ya msongo wa mawazo unahisi itaweza kulishawishi baraza likubaliane na hayo wakati ukijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria?
Bw. Mbowe: Naamini baraza lina majaji wa kutosha wenye taaluma na wanajua uzito wa suala hili, siwezi kuwapangia maamuzi.
Baada ya kumalizika kwa utetezi huo Jaji Lubuva alisema baraza litatoa mapendekeo kwa upande mwingine unaohusika kwa hatua zaidi.
Mbunge mwingine aliyefikishwa jana katika baraza hilo ni Bw. John Komba, mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM) ambaye pia anasubiri uamuzi wa baraza.
Mbowe ni Mwizi huyo anayewanyooshea kidole wenzie,ni muuzaji wa unga,sio aeleze tu pia aeleze alivyozipata na kodi analipa kiasi gani? najua kuna vijibwa vyake vitarukia kumjibia lakini ujumbe umefika
ReplyDeleteJe nawewe ni kijibwa cha nani?,Hebu tufahamishe tuelewe.Kama hauna lakuse bora ukae kimya tu.
ReplyDeleteKumuita kiongozi kijibwa si utu.Dalili zinaonyesha wewe ni wa kile chama kinachokupa ahadi hewa na kukuahidi maisha bora.Mshamba weeeeeeeeeeeee
ReplyDelete