31 May 2011

Mwanafunzi afa kwa mshtuko wa mabomu

Na Heri Shaaban

MWANAFUNZI wa Shule ya Msingi Maarifa, Elizabert John (12), amekufa kwa mshtuko wa mabomu yaliyolipuliwa katika ghala la kuhifadhia silaha la Kikosi cha
511 cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Gongolamboto, Dar es Salaam.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Christophe Mzava amethibitisha kupokea mwili wa mtoto huyo, ambaye alikuwa mkazi wa Gongolamboto Marta.

"Mwili wa mwanafunzi huyo nimeupokea. Kwa sasa hivi hatuwezi kueleza sababu za kifo chake hadi baada ya  uchunguzi baada kukamilika. Anaweza akawa aliogopa mambomu, akakimbia labda akaanguka. Hapo hatuwezi kusema sababu ya kifo bila uchunguzi kwanza," alisema Dkt Mzava.

Naye Ofisa Elimu Manispaa ya Ilala, Tatu Kikwete  alipozungumza na gazeti hili jana mchana kuthibitisha tukio hilo ambalo lipo jirani na shule za msingi, alisema kuwa hatua za awali zilizochukuliwa kurudisha wanafunzi wa shule hizo nyumbani.

Pia aliomba kazi ya ulipuaji mabomu katika eneo hilo ingefanywa kipindi cha likizo baada shule kufungwa kwa kuwa kipindi kina waletea usumbufu wanafunzi.

1 comment:

  1. Jeshi la wananchi Tanzania lina kambi nyingi katika maeneo mbalimbali yanayozunguka nchi na kutokana na fursa hii walionayo kwanini wasitumie kambi ambazo zipo mbali na maeneo walipo wananchi kwa ajili ya kulipua mabomu yao ambayo wanaona hayafai?
    Kuna mambo mengine ambayo yanaepukika ni jinsi ya viongozi wa jeshi kukaa pamoja na kuangalia jinsi ya kuondoa hili tatizo.

    ReplyDelete