Na Addolph Bruno
KLABU 12 za Ligi Kuu zimeanza kunufaika na fedha za matangazo kwa kupewa sh. milioni 6.6 kila moja kutoka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Fedha hizo ambazo ni haki ya televisheni iliyopata nafasi ya kutangaza ligi hiyo ya Sahara Media Group kupitia kituo cha Star TV kwa sh. milioni 14o.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema kutokana na mkataba kati ya kituo hicho na TFF, hadi sasa zimelipwa sh. milioni 100.
Wambura alisema katika mapato yote kila klabu inalipwa asilimia 80 ya malipo hayo ambazo zitalipwa tena mara malipo ya awamu ya mwisho ya sh. milioni 40 yatakapokamilishwa na kituo hicho.
Katika hatua nyingine, Wambura alisema mchezo kati ya Simba na Mtibwa uliochezwa Jumapili katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam umeingiza sh. 39,954,000 kati ya watazamaji 8,609 waliohudhuria.
Wambura pia alisema pambano kati ya Yanga na Ruvu Shooting, lililofanyika juzi katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro limeingiza sh. milioni 11,280,000 kati ya watazamaji 3,760 waliohudhuria pambano hilo.
No comments:
Post a Comment