03 December 2010

'Shibori alicheza chini ya kiwango'

Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa timu ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', John Stewart,  amesema aliamua kumtoa mshambuliaji wake, Ali Ahmad Shibori kutokana na kucheza chini ya kiwango.Mchezaji huyo amejizolea umaarufu hivi kiribuni kutokana na kuonesha kiwango kizuri katika
mchezo kati ya Dar All Stars na Zanzibar Heroes na hata zilipokutana Sudan na Zanzibar Heroes, alitamba kwa kuifungia mabao mawili timu yake.

Kabla ya kukutana na Sudan, klabu ya Simba kutokana na kiwango alichokionesha dhidi ya Dar All Stars,  ilifanya naye mazungumzo na kumsajili kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Ivory Coast, ambapo timu yake ililala bao 1-0, Stewart alisema walikuwa na kila sababu ya kushinda mchezo huo,  lakini bahati haikuwa yao.

"Tulicheza vizuri takribani dakika 60, lakini baada ya kufungwa bao, presha ikahamia kwetu na kujikuta tunahitaji zaidi kushinda wakati tulikuwa tumeshachelewa," alisema.

Akimzungumzia mchezaji Amour Kombo ambaye alikuwa akizomewa na mashabiki na kuamua kumtoa na kumwingiza Hamis Mcha, alisema ni mchezaji mzuri mwenye uzoefu, lakini  alicheza kwa hofu.

Alisema alishindwa kumwingiza mapema Mcha, licha ya kuwa ni mchezaji mzuri kutokana na kutokuwa na uzoefu wa mashindano kama hayo,  lakini anaamini atafanya vizuri zaidi.Zanzibar Heroes itajitupa tena uwanjani leo kwa kuumana na Rwanda ikitanguliwa na mchezo kati ya Somalia na Zambia.

3 comments:

  1. Wa moja wa moja na wa mbili wa mbili tu. Wazanzibari tushazoea kushika mkia. Wache tuendelee tu.

    ReplyDelete
  2. Tanzania na zanzibar bado soka lao changa;;;
    wangati-oman

    ReplyDelete
  3. Acheni wawakomeshe mnajifanya mnajua soka kumbe hamna lolote,huyo shiboli wenu hana lolote bali ni mfukuza upepo uwanjani, wamewaletea nyumbani kikombe sasa kinachukuliwa na nchi nyingine. hakuna soka tz zanzibar subirini kuchwapwa na Rwanda, mfungashe kwenda visiwani kuogelea.

    ReplyDelete