23 December 2010

Eto'o: Mimi si bora kuliko wengine

CAIRO, Misri

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto'o amekataa kwamba yeye ndiye mchezaji bora kuliko wote barani Afrika, licha ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji bora wa mwaka mara nyingi.Mshambuliaji huyo
wa timu ya Inter Milan mwenye umri wa miaka 29, alikabidhiwa tuzo hiyo juzi  kutokana na mafaniko aliyoyapata akiwa na klabu yake.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Cameroon kwa sasa ndiye anashikilia nafasi ya kwanza kwa kutwaa medali nyingi, kuliko mchezaji yeyote barani Afrika."Sidhani kutwaa tuzo mara nne inifanye niwe na haki ya kusema kwamba mimi ndiye mchezaji bora kuliko wote," alisema wakati akiwa mjini Cairo.

"Kuna wachezaji wengi katika kizazi tofauti, ambao wanaleta changamoto na upinzani kwangu. Huwezi kulinganisha na hali halisi," aliongeza na akasema kwamba kuna chipukuzi ambao wanafukuzia mafanikio yake kwa nyuma na wanakuja kwa kasi.

Alisema tuzo hiyo si kitu ambacho kinaweza kukuvimbisha kichwa na ukajiona ni bora kuliko wengine na inapopewa inakupa presha kubwa.

1 comment: