Na Fatuma Rashid
Wadau wa michezo nchini, wametakiwa kujitokeza kuisaidia timu ya
taifa ya vijana ya mpira wa miguu ya wanawake (The Tanzanite), ili iweze kufika
mbali zaidi.
Timu hiyo inakabiliwa na mechi ya marudiano
ya kusaka tiketi kucheza Kombe la Dunia la vijana kwa wanawake, dhidi ya
Msumbiji wikiendi ambapo katika mechi ya awali iliyochezwa wiki mbili
zilizopita Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ilishinda mabao 10-0.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na
wachezaji wa The Tanzanite, wakati wa kuiaga timu hiyo iliyoondoka jana kwenda
Msumbiji Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Juliana Yasoda alisema
timu hiyo inahitaji nguvu za ziada kutoka kwa wadau mbalimbali, ambao
wataisaidia kufika mbali zaidi.
Yasoda alisema timu
hiyo itazidi kusonga mbele kama wadau hao,
watajitokeza kuipa sapoti katika michuano mbalimbali.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu hiyo,
Rogasian Kaijage alisema kikosi chake kipo imara kwa ajili ya mpambano na
watajitahidi kufanya vizuri zaidi ya mechi iliyopita.Kaijage alisema Watanzania
wanatakiwa kuiangalia timu hiyo kwa mtazamo tofauti, kwani hivi sasa anaiandaa
ili kukuza soka la wanawake nchini.
“Hii ni timu ambayo inatakiwa kutazamwa kwa
mbali zaidi, kwani lengo hasa si kwa miaka ya sasa bali ni kuunda soka la
wanawake ambalo litaitangaza Tanzania
katika ramani ya Dunia hapo baadaye,” alisema.
Alisema kuchelewa kwa wachezaji wanne
watakaoungana na wenzao kesho mara baada ya kumaliza mitihani ya kidato cha
nne, haitaathiri kitu kwani watafika ikiwa bado muda wa michuano na pia kama itatokea dharura ambayo itawalazimu kuchelewa zaidi
basi kuna wachezaji wengine ambao pia wanauwezo
No comments:
Post a Comment