Na Namkeshe Ridhiwani
Miss Universe Tanzania,
Betty Omara ametamba katika maonesho ya mavazi kwa warembo 85, wanaowania taji
la Miss Universe 2013 yatakayofanyika mjini Moscow, Urusi.
Katika maonesho hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Vegas Mall, vazi la Betty
lililobuniwa na mbunifu anayekuja kwa kasi nchini, Mwanakombo Salim lilipendwa
na mashabiki wengi na anamatarajio makubwa kushinda taji hilo, wakati wa
fainali za mwaka huu zilizopangwa kufanyika Jumamosi.
Vazi hilo limechorwa na
wasanii wa Tingatinga, Said Kambili na Mimus, michoro ambayo ni maarufu nchini
iliyoasisiwa na msanii maarufu wa zamani, hayati Edward Tingatinga. Vazi hilo mbali ya kudumisha utamaduni wa Tanzania, pia
limechorwa michoro mbalimbali ya kuvitangaza vivutio vya kitalii.
Vazi hilo pia lina nakshi za
mkeka na miba ya mnyama ajulikanaye kwa jina la Nungunungu. Vilevile pia
umetumika kama njia ya kumuonesha ndege tausi kama
inavyoonekana rangi za mkeka kwenye mkia na kilemba kichwani mwake.
Lengo kuu la nguo na
michoro hiyo ni kutangaza kazi za mikono na utalii wa Tanzania na miongoni mwa
michoro iliyooneshwa ni duma, tembo na twiga vilevile imeonesha ndege na
maliasili zipatikanazo Tanzania kama vile tausi, vipepeo, mimea na Mlima
Kilimanjaro.Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na hifadhi
ya Taifa Tanapa
No comments:
Post a Comment