Na Mwandishi Wetu
Kocha raia wa Ufaransa aliyefurushwa Simba msimu uliopita, Patrick
Liewig hatimaye jana amelipwa nusu ya fedha anazoidai klabu hiyo.
Simba imemlipa kocha huyo
dola 10,000 za Marekani kati ya dola18,000 alizokuwa anaidai ambazo imeahidi
kuzilipa wakati mwingine. Kocha huyo anaidai Simba fedha hizo kwa ajili ya
kuifundisha timu hiyo kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu, ambapo nafasi yake imezibwa
na Mzalendo Abdallah ‘King’ Kibadeni.
Akizungumza mara baada ya kumkabidhi
fedha hizo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang are Kinesi alisema kocha huyo atalipwa fedha nyingine leo kiasi cha dola 3,000 na
nyingine atalipwa mwakani ambazo ni dola 5,000.
Kocha huyo ambaye alikuwa akiidai Simba dola
26,000 tayari alishalipwa dola 10,000 Juni mwaka huu. Liewig alikuwa anadai dola
12,000 za mshahara wake na dola 12,000 kwa ajili ya kuvunjiwa mkataba wake na
dola 2,000 za tiketi za kwenda kwao Ufaransa.Liewig aliiongoza Simba katika mechi
25 ambapo kati ya hizo ishinda tisa, sare nane na kufungwa saba.
No comments:
Post a Comment