Na Mariam Mziwanda
Kufuatia maadhimishoyawiki ya m lipakodi nchi ni, Mamla ka yaMapato
Tanzania(TRA)imew aelezaw ananchi kuwaita endele akufanyaka zizake k wauwazina
uwajibik ajiili kupan ua wigow ahudum akw ajamiinakuwez aku jengatai fala
walipak odikwahiyari
. Hayo yalis emw
a janajijini Dar es Salaa mkatika maonyes hoy amlipakodikw enyeviwanjavy aM
nazi Mmoja na ofisa elimu na huduma kwa mlipa kodi TRA Bw.Sigsimund Kafuru na
kusisitiza kuwa lengo la kuwa karibu na wananchi ni kuwawezesha kutambua
utendaji wa TRA katika huduma za ulipaji kodi.
Alisema katika
maonyesho hayo ikiwa ni wiki ya mlipa kodi nchini TRA imenufaika na kutambua
michango ya wadau mbalimbali.
"Hakuna
taifa linaloweza kuendelea pasipo walipa kodi kwa kutambua hali hiyo TRA
kupitia maonyesho haya tumekuwa karibu zaidi na wananchi na tumefanikiwa kupata
michango yao ikiwemo maoni, mawazo na ushauri lakini pia tumeweza kutoa elimu
kwa kundi kubwa la wananchi hatua ambayo wengi wao imewaondoa woga juu ya
utendaji wa kazi zetu ambazo zinahitaji ushirikiano," alisema.
Alieleza kupitia maonyesho
hayo pia wamewawezesha wananchi kujua ulipaji wa viwango vya kodi, utaratibu wa
bidhaa sambamba na mfumo wa matumizi ya ulipaji kodi kwa njia ya mashine za
electronic, ulipaji wa kodi wa leseni za magari kwa njia ya mtandao na huduma
za benki.
Bw. Kafuru alisema lengo la TRA kurahisisha
zaidi huduma zake ni kuona kila mwananchi anafikiwa katika ulipaji wa kodi kwa
unafuu hivyo ametoa wito kwa jamii kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanakuwa
miongoni mwa watoa risiti na wadai risiti ili kuweza kuongeza pato la taifa kwa
mustakabali wa maendeleo nchini.
No comments:
Post a Comment