Na Ester Maongezi
Timu ya Simba jana ilimaliza mzunguko wa
kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuibamiza Ashanti
United, mabao 4-2 katika mechi ya ligi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo
hayo Simba imefikisha pointi 24 ikiwa nafasi ya nne nyuma ya Yanga yenye pointi
25 huku, Amis Tambwe akifikisha mabao 10 baada ya kuifungia timu hiyo bao
katika mechi hiyo.Katika msimamo
wa ligi hiyo, Azam FC inaongoza ikiwa na pointi 26 sawa na Mbeya City ambayo
nayo ina idadi ya pointi kama hiyo isipokuwa inazidiwa kwa mabao ya kufunga na
kufungwa, huku Yanga ikikamata nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 25.
Simba ambayo
jana iliingia uwanjani ikiwa na uchu wa mabao ilipata bao la kwanza dakika ya
saba kupitia kwa mshambuliaji wake hatari, Ramadhan Singano ‘Messi’ baada ya
kuwachambua mabeki wa Ashanti.Ashanti baada ya kufungwa
bao hilo
ilikuja juu ambapo dakika ya 22, Said Maulid alikosa bao la wazi baada ya
kubaki na kipa lakini akashindwa kufunga.
Maulid aliikosesha tena
bao Ashanti,
dakika ya 31 baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Fakih Hakika, lakini
mshambuliaji huyo mkongwe akashindwa kukwamisha mpira wavuni.Simba baada ya
kushambuliwa mfululizo ilizinduka kutoka usingizini ambapo dakika ya 37, Amri
Kiemba alikosa bao la wazi baada ya kupata pasi ya Jonas Mkude.
Dakika ya 44 Singano
aliikosesha Simba bao la wazi baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Tambwe,
lakini shuti la mshambuliaji huyo likadakwa na kipa wa Ashanti.Ashanti ilisawazisha bao hilo dakika ya 45 kupitia
kwa Hussein Sued, baada ya kuitumia nafasi vizuri aliyoipata.
Kipindi cha pili
kilianza kwa Simba kulishambulia lango la Ashanti ambapo dakika ya 46, Tambwe
aliipatia Simba bao la pili baada kuunganisha vyema krosi ya Singano ambaye
jana alikuwa nyota wa mchezo.Dakika ya 49, Betram
Mombeki aliiandikia bao la tatu Simba akiunganisha krosi ya Singano kutoka
wingi ya kulia.
Maulid aliipatia
Ashanti bao la pili dakika ya 52 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliokwenda
moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa wa Simba akigaagaa bila mafanikio.Simba ilihitimisha
bao la nne dakika ya 60 kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya beki wa kulia,
Haruna Shamte aliyepanda mbele kuongeza mashambulizi.
Naye Omari Mngindo
anaripoti kutoka Uwanja wa Mabatini Mlandizi kuwa, Timu za Mtibwa na Ruvu Shooting zilitoka sare katika mfululizo wa
mechi hizo za ligi kuhitimisha raundi ya kwanza.
Ligi hiyo inatarajia kuchezwa tena leo ambapo Yanga itaumana na JKT
Oljoro katika Uwanja wa Taifa, huku Azam FC ikiwa wenyeji wa Mbeya City kwenye
Uwanja wa Azam Complex Chamazi uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment