- AZUNGUMZIA TUHUMA DHIDI YAKE NDANI YA CCM
- ATOA MSIMAMO URAIS 2015, AMUUNGA MKONO JK
Vita ya kuwania urais ndani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), inazidi kupamba moto baada ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu wa
Tatu, Bw. Frederick Sumaye, kuanika hujuma zinazofanyika dhidi yake kupitia
mialiko, usambazaji taarifa katika vyombo vya habari na propaganda chafu za
kisiasa.
Bw.
Sumaye alianika hujuma hizo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi
wa habari juu ya hujuma anazodai kufanyiwa pamoja na kutoa msimamo wake wa
kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, kwa kukemea rushwa
ndani ya chama hicho.
Alisema zipo hujuma zinazofanywa katika
shughuli za jamii kwa masilahi kisiasa ambapo kuna mialiko inayotolewa na
taasisi, vikundi vya jamii au madhehebu ya dini kwa viongozi mbalimbali ili
waweze kuwasaidia katika shughuli zao kama
kuhamasisha, kutoa ujumbe, kuzindua jengo, mradi pamoja na kuchangia fedha.
Aliongeza kuwa, mwaliko uliopangwa unaweza
kuvurugwa kwa sababu yoyote ambayo haistahili kuwepo na kusababisha wahusika
kucheleweshewa maendeleo na manufaa ambayo wangeyapata kutokana na shughuli inayohusiana na mwaliko huo.
Alitoa mifano
miwili iliyohusu kujuma dhidi yake na kudai Oktoba 27 mwaka huu, alialikwa na
kikundi cha Joggers cha Dar es Salaam, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja."Dakika
za mwisho, nilipewa taarifa kuwa shughuli imeshindikana kwa sababu imeingiliwa
na kikundi chenye kulinda masilahi yake au ya mtu wao lakini baadaye niliambiwa
ilifanyika na mgeni rasmi alikuwa mtu mwingine," alisema Bw. Sumaye.
Alisema hiyo
ilikuwa mbinu ya kuzuia ujumbe aliokusudia kuutoa siku hiyo ambapo hujuma ya
pili, ilihusu mwaliko wa kuzindua SACCOS ya Nshamba Muleba, mkoani Kagera,
ambapo alipata mwaliko wa kufanya shughuli hiyo Oktoba 28 mwaka huu.
"Mwaliko
huu sikuuomba bali viongozi wa chama walinipendekeza kwa sababu zao wenyewe
sasa wakati najiandaa kwenda Kagera, nikaambiwa shughuli zimeingiliwa na watu
fulani ambao walitoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa SACCOS ili isifanyike na
kuambiwa haiwezekani Sumaye afike Kagera kabla ya mtu wao," alisema Bw.
Sumaye na kuongeza;
"Hata
matangazo yaliyolipiwa fedha kutangaza mkutano huo, ilibidi yasitishwe na fedha
kurudishwa...nataka kuwaambia hao wanaohangaika na mialiko yangu wajue kuwa,
mialiko ninayo mingi hadi mingine nakosa muda wa kwenda, siitwi kwa sababu ya
fedha maana wanajua sina fedha za aina hiyo," alisema.
Bw. Sumaye
alisema, jinsi wanavyojitahidi kumzima kwa rushwa ili asiendelee kukemea
vitendo hivyo, ufisadi na dawa za kulevya ndivyo wanavyompa nguvu na mifano hai
ya jinsi rushwa na ufisadi ni kirusi hatari katika Taifa.
Alisema
mafisadi ni watu hatari katika jamii kwani lengo ni kuvuruga mipango ya nchi.
Aliongeza
kuwa, kipindi hiki cha kuelekea 2015 kuna propaganda na mbinu mbalimbali
zinazotumika na wanasiasa wanaotafuta nafasi mbalimbali kufanikisha malengo yao.
Alisema kuna
mbinu nzuri za kistaarabu pia kuna mbinu chafu kama
za kupakazana matope.Bw. Sumaye alisema mbinu ya kistaarabu ni pale mhusika
anapowashawishi wanaomsikiliza kuwa yeye ni mtu safi atakayemudu nafasi hiyo bila kumwathiri
mtu mwingine ambaye anadhaniwa kuwania nafasi husika.
"Mtu wa
aina ya kwanza, tungeweza kusema anajisafishia njia yake kwa kufyeka miiba na
kuondoa magogo njiani ili wakati ukiwadia mbio zake zisikwazwe na vigingi
vyovyote."Aina ya pili ni mbinu chafu ambapo mhusika anatengeneza mbinu za
kuwamaliza wengine wanaodhaniwa kuwa washindani wake au kuwawekea vikwazo
wasijisafishie njia," alisema.
Alisema mtu wa
aina hiyo anawachafua wenzake kwa kuwapakaza matope ya uongo au kuwajengea
mazingira yeye kupendwa kwa kutumia migongo ya wengine.Tukirudi kwenye mfano
wetu wa kufyeka barabara, atakuwa anachimba mitaro kwenye barabara wanazofyeka
wenzake au anatupia miba na magogo yanayotoka kwake na kuyatupia kwa wenzake
ili mradi wenzake wakwame wakati ukiwadia.
"Mimi mtu akihangaika kujisafishia njia
bila kuathiri wengine au kuathiri mambo fulani ya msingi huwa hainisumbui sana, lakini ikiwa inaathiri mtu mwingine itabidi tuiambie
jamii ukweli na hivi ndivyo nitakavyofanya leo (jana), hata wakati mwingine
jambo kama hilo
likijitokeza," alisema Bw. Sumaye.
Alitolea mfano
habari moja iliyoandikwa na gazeti moja (si Majira) kuwa Siri ya mradi wa
kuvuta maji Ziwa Victoria
yafichuliwa.
Aliongeza
kuwa, katika maelezo yake mtoa habari alisema ni Mawaziri wawili tu waliounga
mkono mradi huo na wengine waliupinga."Najua mhusika ameutumia mradi huu
kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua sana ili la mradi ametukanyaga vidole wengine
na kutupia miba na magogo kwenye njia yetu.
"Amenilazimisha
niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa Waziri Mkuu na
mradi umetekelezwa chini ya uangalizi wangu kama
kiongozi na Msimamizi Mkuu wa utekelezaji wa shughuli zote za Serikali.
"Kama unachumbia
msichana mzuri mweleze jinsi utakavyomjengea nyumba, lakini usianze kuwachafua
wengine wanaotaka kumchumbia msichana huyo," alisema.Bw.Sumaye alisema
lililoelezwa kuhusu mradi huo ni uongo, mhusika kama Waziri Mwandamizi wakati
huo na sasa anadaiwa kuwinda nafasi kubwa katika nchi, hakutegemewa kutoa siri
za Baraza la Mawaziri labda amediriki kufanya hivyo kwa sababu anajua
anayoyasema siyo ya kweli vinginevyo ni kosa la jinai na akishtakiwa anafungwa
jela.
Aliongeza
kuwa, mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria
ni mradi wa Serikali si wa mtu. "Mradi huu ulikuwa wa Mheshimiwa (jina
tunalihifadhi), wakati huo alikuwa Waziri wa Maji na aliusimamia hadi
ukakamilika kama ambavyo angeusimamia Waziri
mwingine wa Maji.
"Nataka ieleweke wazi kuwa hakuna Waziri
mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kama baraza
la Mawaziri likiukataa, alisisitiza na kuongeza kuwa, hapendi kuingilia mambo
ya watu wengine lakini yanapomgusa hatanyamaza hivyo ni wajibu wake kueleza
ukweli hasa pale unapopotoshwa kwa makusudi.
Kumuunga
mkono JK
Bw. Sumaye alisema anamuunga mkono Rais
Kikwete kwa kuonesha nia ya kupambana na rushwa ndani ya chama hicho kwani yeye
ataendelea kuwa mstari wa mbele katika vita hivyo. Alipoulizwa atafanya nini kama watu wanaotoa rushwa watapitishwa na CCM kuwania
uongozi, alisema; "Kama CCM itapitisha majina bila kuangalia waliotoa
rushwa chama kitaanguka.
"Lakini siamini
kuwa watapitisha watu wanaonunua watu wengine, wakipitisha hatutaweza kukaa
pamoja na watoa rushwa, sitahama, lakini sitakaa nao," alisema.
Kuwania
Urais
Alipoulizwa kama ana mipango ya
kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu 2015, Bw.Sumaye alisema;
"Mimi ni mwana CCM, chama kimesema atakayejitangaza atakiona
cha moto, sasa mnataka nikione cha moto...kama
ni kugombea nina haki zote, uwezo na nina imani Watanzania wana imani na
mimi," alisema.
Alisema amekuwa akisikia watu wakimtaja
lakini wakati ukifika atatangaza kama anawania
nafasi hiyo au hapana.
Fedha
UswisiAlipoulizwa kama yeye ni miongoni mwa watu waliohifadhi
fedha nje ya nchi hususan Uswisi, alikataa na kuishangaa Serikali kwanini
inashindwa kuwataja watu hao.
"Sijawahi kuwa na akaunti nje hata ambayo
haina hela lakini nashangaa kwanini Serikali haifanyi utaratibu kwa ajili ya
kuwataja majina walioficha fedha huko," alisema Bw. Sumaye.
Jumuiya ya
Afrika Mashariki
Bw.
Sumaye alisema ni kosa kubwa kwa Tanzania
kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwani suala hilo ni la wananchi si la viongozi.Alisema
katika ulimwengu wa sasa, nchi nyingi zinaungana hivyo suala la kujitoa ni la
wananchi kuamua wenyewe kwani wakati wa kuanzishwa tena jumuiya hiyo walikaa
vikao vingi na wananchi ndipo waliporidhia.
Aliongeza kuwa, nguvu kubwa ilitumika wakati
wa kuanzishwa jumuiya hiyo ambayo awali ilivunjika lakini anashangaa kuona kuna
watu wanataka kujitoa kitu ambachoki namu umiza sana."Dunia nikotenchim balimbali
zinaungana, hakuna uchumi unaoendeshwa kwa malori ila kuimarika kwa reli na bandari
kutaifanya Tanzania
kuwa na uchumi mkubwa kwa haraka.
"Huwezi kutegemea uchumi unaotokana na jembe
la mkono bila kuimarisha banda rina reli, usafiri wa rel I ndio muhimu katika
usafirishaji,"alisema Bw. Sumaye. Aliongeza kuwa, kauli zinazotolewa na baadhi
ya viongozi ku wa Tanzania
ina eneo kubwa na wengine kudai watatoa talaka zinamshangaza kwani katika maeneo
mengi h ususan mkoani Arusha,ardhi kubwa imechukuliwa na wageni wakiwemo Wachina.
"Kwa maoni yangu, napingana na Tanzania kujitoa
Afrika Mashariki kwa sababu nchinyin gi duniani zina unganalak
iniwenginewanasema sisi ndiyo tutatoa talaka," alisema.Alisema njia pekee ni
kukaa katika mazungu mzo ili kutatua changamoto zilizopo kwani kama nchi ina
bandari ni kitu muhimu sana hivyo kusema waende kujiun gana C ongo(DRC) ni
kitukisichokubalika
No comments:
Post a Comment