Na
Ester Maongezi
Klabu yenye ushindani kwenye Ligi Kuu
Tanzania Bara ya Mbeya
City imesema haiiogopi
Azam FC na kwamba ipo tayari kuvaana nayo hapo kesho.
Timu hizo ambazo zina pointi 26 zote
isipokuwa Azam inaongoza kutokana na kuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga
na kufungwa,zinatarajiwa kumenyana kesho katika Uwanja wa Chamazi Complex nje kidogo
ya jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwa
simu jana Msemaji wa Klabu ya Mbeya
City, Fred Jackson alisema
wapo tayari kucheza na Azam na hawaiofi i hata kidogo.Jackson
alisema hawaigopi Azam, ila wanaipa uzito kama
walivyofanya katika timu walizowahi kukutana nazo katika ligi.
“Hatuiogopi
Azam ila tunaipa uzito kama moja ya timu
nzuri, ambazo tunakutana nazo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka
huu, ila sisi kama Mbeya City tumejiandaa vya kutosha,” alisema Jackson.
Jackson
aliongeza kuwa wanakiamini kikosi chao kutokana na kwamba hawana majeruhi hata mmoja.
Mbeya City
inatarajia kuingia jijini Dar es
Salaam leo wakitokea Mbeya tayari kabisa kwa ajili
kuivaa Azam kesho.
No comments:
Post a Comment