Na Fatuma Rashid
Pazia la michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), mzunguko wa
kwanza linafungwa leo kwa mechi tano kupigwa viwanja tofauti nchini.
Katika mechi hizo Simba
yenye pointi 21 inayoshikilia nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo itakuwa
wenyeji wa Ashanti United katika
mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Simba itaingia uwanjani
ikisaka pointi tatu kwa udi na uvumba, baada ya kushindwa kufanya hivyo katika
mechi nne zilizopita ambapo ilitoka sare tatu na kufungwa moja.
Ashanti United imefikisha pointi 10
na kushika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14.JKT Ruvu
inayoshikilia nafasi ya 9 naye itashuka katika Uwanja wa Chamazi Complex
kuumana na ‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union inayoshika nafasi ya 7
kwa kuwa na pointi 16.
Nayo Kagera Sugar
itaikaribisha Mgambo Shooting katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba..Kwa upande
wake Rhino Rangers yenye pointi 11 iliyopo nafasi ya 10 watawakaribisha Tanzania
Prisons yenye pointi 8 ikiwa nafasi ya 12 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini
Tabora.
Nayo Ruvu Shooting wakiwa
na pointi 14 iliyopo nafasi ya nane, watajitupa katika Uwanja wa Uwanja wa
Mabatini kuikaribisha
Mtibwa Sugar ambayo ina pointi 19 wakiwa nafasi ya tano.Timu zote zinapigana kuhakikisha
zinapata pointi tatu muhimu, ili kujiweka vyema katika msimamo wa ligi hiyo
No comments:
Post a Comment