07 November 2013

JK KUHUTUBIA BUNGE DODOMA LEO



Na Mwandishi Wetu

  Rais Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, hotuba ambayo inasubiriwa kwa hamu na wananchi wengi.Habari zilizopatikana Mjini Dodoma jana na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge pamoja na Ikulu, Dar es Salaam, zinasema atahutubia mchana.

  Shauku ya watu kutaka kusikiliza hotuba ya Rais Kikwete, ni kutokana na ukweli kuwa atazungumzia   mchakato mzima wa mabadiliko ya Katiba
  Habari zinaeleza kuwa Mawaziri na Manaibu Waziri hawatatoka nje ya Dodoma hadi hapo Rais atakapokuwa amehutubia Bunge.Kadhalika safari zote za Kamati za Bunge ambazo zilikuwa katika mchakato wa kutekelezwa zimeahirishwa hadi baada ya kesho, ili kutoa fursa kwa wabunge wote kuwapo wakati wa hotuba hiyo. Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alithibitisha kuwa Rais Kikwete atalihutubia Bunge, leo.

1 comment:

  1. Mh. Kikwete,
    Suala la shirikisho AM haliwezekani kutokana na sababu nyngi baadhi kama zifuatazo:
    1. Viongozi wake wanatawala kimabavu labda kuondoa Kenya
    2. Kukosekana kwa demokrasia, vyama tawala vinatawala kama ndivyo viliundwa kutawala. Juhudi zozote za kuviondoa utaitwa gaidi au mchochezi
    3. Viongozi kukumbatia rushwa
    4. Miundo mbinu chakavu
    5. Elimu duni
    6. Hali mbaya ya kiuchumi
    7. Hali ya utegemezi kwa mfano Tanzania hawawezi kuua hata mbu.Matokeo yake wanaomba misaada ya viandarua
    8. Kutojitambua kwamba wanaAM nao ni binadamu. Kwa mfano utamkuta mkurya anajiita John eti Marwa ni jina a kishenzi, kina mama kujichubua waonekane wazungu, na
    9. Kadhalika



    ReplyDelete