Na Fatuma Rashid
Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF), limeteua waamuzi kutoka Burundi
kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya miaka 20
kati ya Tanzania
na Msumbiji
.Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Boniface Wambura alisema waamuzi watakaochezesha mechi hiyo ya kwanza ya
raundi ya kwanza itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Oktoba 26
na 27 mwaka huu wataongozwa na Ines Niyonsara akisaidiwa na Jacqueline
Ndimurukundo na Axelle Shikana.
Wambura alisema,
Irene Namiburu kutoka Uganda
ndiye atakayekuwa mwamuzi wa mezani wakati Kamishna wa mechi hiyo atakuwa ni
Evelyn Awuor wa Kenya.Alisema mechi ya
marudiano itachezwa jijini Maputo, kati ya
Novemba 9 na 10, mwaka huu na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar.
Fainali hizo za Kombe
la Dunia zitafanyika mwakani nchini Canada,
ambapo Tanzania
inashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Kombe la Dunia kwa wasichana.Timu ya Tanzania
tayari imepiga kambi mkoani Pwani ikiwa chini ya Kocha wake Rogasian Kaijage.
No comments:
Post a Comment