Na Neema Ndugulile
Kocha Mkuu wa
Simba, Abdallah Kibadeni amekataa kuwataja majeruhi katika kikosi chake kwa
kuhofia kuhujumiwa na timu pinzani, Ruvu Shooting.
Simba na Ruvu Shooting, zinatarajia kumenyana kesho katika mechi ya Ligi
Kuu Tanzania Bara, inayotarajiwa kupigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana, Kibadeni alisema hawezi
kuwataja majeruhi waliopo katika kikosi hicho kwa kuwa akifanya hivyo atawapa
nafasi wapinzani wao kujipanga.
Licha ya
kocha huyo kukataa kuwataja majeruhi hao alisema ana taarifa ya Miraji Adam,
ambaye aliumia kidole na hajaruhusiwa kufanya mazoezi. Akizungumzia mechi hiyo ya kesho, Kibadeni
alisema itakuwa ngumu hivyo wataingia kwa hadhari ili kutoka na ushindi. "Mchezo
huo unahitaji umakini wa hali ya juu na ndiyo maana tumejipanga vyema
kukabiliana na Ruvu kwa hali yoyote uwanjani," alisema
No comments:
Post a Comment