04 October 2013

WARIOBA AMTOLEA 'UVIVU' BULEMBO

Bw. Abdallah Bulembo


  •  NI KUHUSU TUHUMA ZAKE KWA TUME YA KATIBA
  • ADAI MAZINGIRA YA KAZI YAO NI MAGUMU SANA

Na Mwandishi Wetu

  Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imetoa ufafanuzi juu ya kauli mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya wanasiasa kuwa tume hiyo imekuwa ikiingilia uhuru wa wananchi kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ngazi ya Wilaya iliyomalizika hivi karibuni
.  Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Joseph Warioba, alisema siku zote tume hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwataka wanasiasa kujadili rasimu iliyotolewa badala ya kuhangaika na tume au wajumbe wake

 Moja ya kazi za kisheria za tume ni kutoa elimu kwa umma ambayo ndiyo kazi ya wakati wote," alisema Jaji Warioba wakati akijibu swali la waandishi waliofika ofisini kwake kutaka ufafanuzi wa kauli ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Abdallah Bulembo.

Bw. Bulembo amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akiwa mkoani Tanga na kudai kuwa, tume ya Jaji Warioba imeacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia uhuru wa wananchi wa kutoa maoni.

Jaji Warioba alisema, katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, wananchi ambao ndiyo wajumbe wa Mabaraza hayo, walikuwa na fursa ya kuuliza maswali na wajumbe wa tume walitoa elimu kuhusu hoja na maswali yaliyoulizwa kwa mujibu wa sheria.

"Sasa (Bw. Bulembo) anaona kutoa elimu ni dhambi," alisema Jaji Warioba ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na kusisitiza kuwa, tume yake imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu.

Hali hiyo inatokana na kauli za wanasiasa mbalimbali lakini tume yake bado inafarijika na kauli za kutia moyo ambazo zinatolewa na wananchi wa kawaida.

"Mwezi uliopita, nilisema wanasiasa wamekuwa wakitoa matamshi yaliyoifanya kazi ya tume kuwa ngumu katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba.

"Matamshi mengine yaliilenga tume, wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au wajumbe wa tume badala ya kuzungumzia rasimu," alisema Jaji Warioba ambaye anaongoza tume yenye wajumbe 32.

   Jaji Warioba aliongeza kuwa, siku zote tume yake imekuwa ikikubali kukosolewa ikiamini kuwa, hilo ni jambo la kawaida na kusisitiza kuwa ni vyema wananchi na wanasiasa wakajadili rasimu ya katiba iliyotolewa badala ya watu au tume.

  “Kama wangezungumzia rasimu wangetusaidia sana badala ya kuzungumzia tume na watu," alisema Jaji Warioba na kuongeza kuwa, haamini kama kauli za viongozi hao wa kisiasa ndiyo misimamo ya vyama vyao

4 comments:

  1. NI KWELI JAJI J.S.WARIOBA AMEKUWA KAMA JAJI WA WAWATANZANIA KUHUSU KATIBA YEYE ABAKIYE UPANDE KATI KATI NA SIYO KUSHABIKIA UPANDE MMOJA MFANO WA SEREKALI TATU.JAJI AMEKUWA WAZI KUWA ANATAKA SEREKALI TATU NA AMEONEKANA KUPINGANA NA CCM MOJA KWA MOJA KITU AMBACHO HAKIPENDEZI KWA MWENYEKITI KUWA KINGANGANIZI WA ANACHOPENDA YEYE.AMESAHAU KUWA YEYE SIYO JAJAI KWENYE KATIBA BALI NI MWENYEKITI WA KUKUSANYA MAONI YA WATANZANIA NA SIYO KUYATOLEA MAAMUZI.

    ReplyDelete
  2. INASIKITISHA SANA KUONA KUWA UELEWA WA NINI KINATAKIWA KUFANYIKA BAADHI WANADHANI WAO NI WAHUSIKA SAHIHI NA WENGINE SIO WAHUSIKA...JIBU NI KUWA KILA MTANZANIA ANAYO HAKI YA KUTOA MAONI..JAJI WARIOBA NI MTANZANIA MWENYE HAKI BINAFSI NA MWENYEKITI MUELIMISHAJI UMMA KISHERIA..NI WAJIBU WAKE KAMA ILIVYO KWA KILA MTANZANIA KUTOKUWA MNAFIKI WA KUTOA MAWAZO BALI MUWAZI NA MKWELI KWA MAZINGIRA YALIYOPO KWA MUSTAKABALI WA WANAINCHI WOTE BILA KUJALI VYAMA. DINI, RANGI, KABILA NK-JAJI ANATOA MAONI NA ELIMU KWA WATANZANIA WASIOELEWA VEMA SERIKARI MOJA , MBILI, TATU NI NINI, NA SIO MAAMUZI...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukipendekeza serikali tatu ni vyema utangaze kuwa muungano haupo!

      Delete
  3. Kwani muungano upo kwa sasa?, naona yapo maandishi tu kuwa bara wameungana na Zanzibar, wana bendera yao vitambulisho vyao bunge lao wawakilishi

    ReplyDelete