Wanawake na wanaume wanaopenda kujichubua, wapo hatarini kupata
ugonjwa wa ukoma kutokana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali, anaripoti
Elizabeth Joseph, Dodoma
Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma mkoani Dodoma, Dkt. Martin
Massimba, aliyasema hayo mjini humo jana wakati akizungumza na Majira juu
ya athari zitokanazo na matumizi ya vipodozi kwa wanawake na wanaume wanaopenda
kujichubua.
Alisema baadhi ya wanawake na wanaume wana
tabia ya kutumia vipodozi vikali kwa kuvichanganya na kemikali nyingine ili
waweze kujichubua.
“Wote wanaofanya hivi wapo katika hatari ya
kupata ugonjwa wa ukoma, vipodozi vingi wanavyotumia kuvichanganya vina kemikali
nyingi zinazoweza kuharibu ngozi yao,”
alisema.
Aliongeza kuwa, watumiaji vipodozi
wanapotokewa mabaka katika ngozi zao, hudhani y ame t o k a n a n a v i p o d o
z i walivyotumia jambo ambalo si kweli, bali wengi wao waliopima, vipimo
vimeonesha kuwa na ugonjwa wa ukoma.
Dkt. Massimba alitoa wito
kwa watu wote wanaopenda kutumia vipodozi vyenye kemikali kali, kuacha mara
moja pia kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujua kama wana maambukizi ya ugonjwa huo ambao huchukua muda
mrefu hadi kujulikana
No comments:
Post a Comment