Mkazi wa Kijiji cha
Bitale, Wilaya ya Kigoma Vijijini, amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla
wakati akitoa ushahidi kwenye Mahakama ya Mwanzo, iliyopo Mwandiga, mkoani
Kigoma, anaripoti Mwajabu Kigaza, Kigoma.
Tukio hilo limetokea Oktoba 17 mwaka huu, saa
nne asubuhi na marehemu amefahamika kwa jina la Yusuph Kazirai (65).Akizungumzia
tukio hilo, Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Bw. David Ngunyale, alisema
marehemu alikuwa mlalamikaji katika kesi ya jinai namba 94 ya mwaka 2013.
Alisema wakati marehemu
akitoa maelezo yake juu ya kesi hiyo mbele ya mahakama, ghafla alianza kuishiwa
nguvu, kuanguka chini ambapo baada ya kuwahishwa hospitali na kufanyiwa vipimo,
ilithibitika tayari amefariki dunia.
No comments:
Post a Comment