Na Penina Malundo
Imeelezwa kuwa Tanzania
imeendelea kufanya vizuri kiuchumi katika nchi za Afrika Mashariki
ukilinganisha na Kenya, Rwanda, Uganda
na Burundi
. Akitoa takwimu hizo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke wakati akizungumza na waandishi wa habari
juu ya ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya Pili ya Mwaka 2013, alisema Tanzania
inashikilia nafasi ya pili.
Oyuke alisema kuwa, moja ya Sababu inayofanya
uchumi wa nchi kukua kulinganisha na nchi nyingine ni pamoja na Serikali
kuongeza nguvu katika kuwekeza ukuaji wa shughuli za uchumi wa kilimo nchini.
“Serikali inatumia Sera zake katika kukuza
uchumi wa nchi, kwa kutumia sekta yenye watu wengi, kama
ya kilimo, kwani asilimia kubwa ya wananchi wanawekeza katika kilimo huku mvua
nazo zimekuwa za kutosha katika mikoa inayozalisha mazao mengi na kufanya
wakulima kuwa na mazao mengi ya biashara pamoja na ya chakula,” alisema Oyuke.
Alisema kuwa, katika nchi za Afrika Mashariki
nchi inayoongoza katika ukubwa wa uchumi ni Kenya
ikifuatiwa na Tanzania hivyo
uzalishaji hapa nchini umekua kwa kiasi kikubwa kuliko nchi ya Uganda, Rwanda
pamoja na Burundi.
“Sisi ni wa pili katika ukuaji wa uchumi wa
nchi kwa nchi zote za Afrika Mashariki ikiongozwa na nchi ya Rwanda na kwa
ukubwa wa uchumi wa nchi. Kenya
inaongoza tukifuatiwa na sisi, Uganda,
Rwanda pamoja na Burundi,”
alisema Oyuke.
Aliongeza kuwa Pato la Taifa limeweza
kuongezeka kwa robo ya pili ya mwaka 2013 kutoka asilimia 6.4 kwa robo ya mwaka
2012 hadi kufikia asilimia 6.7 kwa mwaka huu.
Alisema kuwa, ukuaji wa
pato la taifa unatokana na uboreshwaji wa sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya
kilimo, uvuvi, viwanda, ujenzi pamoja na nishati.
No comments:
Post a Comment