Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya
Mawasiliano Tanzania (TTCL) imejidhatiti kupambana na udanganyifu unaofanywa na
baadhi ya watu kupitia mitandao ili kuwahakikishia wateja wake huduma bora.
Kauli hiyo
ilitolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Dkt. Kamugisha Kazaura, wakati
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa warsha ya
wataalamu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi
karibuni.
Dkt. Kamuzora alisema kuwa TTCL ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya ulinzi
na mbinu za kukabiliana na wizi na udanganyifu katika mitandao, hivyo
kuwakikishia wateja wake huduma bora.
"Tunalazimika
kuwa na mbinu za ziada hata kama wahalifu
wanaweza kuwa na utaalamu zaidi yetu," alisema Dkt. Kazura.
Aliongeza kusema kuwa tatizo la wizi na udanganyifu kwa njia ya mtandao
ni kubwa na linahitaji kuwepo kwa sera ya udhibiti ya matumizi ya mtandao wa
ndani, nje na hata katika ngazi ya kimataifa.
"Uhalifu wa mtandao ikiwemo wizi na udanganyifu ni tatizo ambalo
hatupaswi kudhrau, ni kama ugonjwa unaohitaji
tiba," alisema Dkt. Kazaura.
Alisema kuwa mkutano huo ulilenga kuja na mapendekezo ya kudhibiti
tatizo hilo
katika jumuiya. "Tumekutana kuzungumzia wizi na udanganyifu wa mitandaoni
na usalama wa mitandao hii na mapendekezo yatakayotolewa yatafikishwa kwenye
mkutano wa Mawaziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)," alisema.
TTCL ni moja ya taasisi zinazotakiwa kuhakikisha tatizo hilo
linapungua na kuisha kabisa kutokana na jukumu lake kubwa
la kusimamia Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ambao kupitia kwake huduma za
kimtandao zimeshaanza kutolewa ndani na nje ya nchi.
Alisema kuwa nchini Tanzania Mkongo wa Taifa umeboresha huduma za
mawasiliano na kusaidia kuboresha huduma za mawasiliano kwa kutumia mitandao
mbalimbali ikiwemo ya intaneti.
Kupitia mitandao hiyo watu
hutuma na kupokea fedha, pia hupata taarifa mbalimbali, sasa baadhi ya watu
hutumia fursa ya kukua kwa tehama kufanya wizi na udanganifu huo mitandaoni
No comments:
Post a Comment