Na Fatuma Rashid
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF),
imefanya marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ili kupisha mechi
ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania na Msumbiji.
Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
alisema kuwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza kwa mashindano ya
wanawake wenye umri chini ya miaka 20 itachezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa
10 jioni.
Wambura alisema
kuwa,timu hiyo chini ya miaka 20 tayari imehamishia kambi yake hosteli ya Msimbazi Center,
Dar es Salaam
kutoka JKT Ruvu mkoani Pwani tangu wiki iliyopita kujiandaa kwa mechi hiyo.
Fainali za Kombe la
Dunia kwa U20 wanawake zitafanyika mwakani nchini Canada.Alisema kuwa,
marekebisho ya ratiba ya VPL yamegusa raundi zote tatu zilizobaki kukamilisha
mzunguko wa kwanza.
Ambapo alisema kuwa
kutokana na marekebisho hayo mechi za raundi ya 11 zitakuwa ifuatavyo; Oktoba
28 mwaka huu ni Coastal Union vs Mtibwa Sugar,
Oljoro JKT vs Ashanti United, Ruvu Shooting vs Kagera Sugar na Simba vs Azam.
Oktoba 29 mwaka huu
ni Tanzania Prisons vs Mbeya
City, Yanga vs Mgambo
Shooting na Rhino Rangers vs JKT Ruvu.Raundi ya 12 ni kama ifuatavyo; Oktoba 31 mwaka huu ni Simba vs Kagera
Sugar, Novemba mosi mwaka huu ni JKT Ruvu vs Yanga.
Novemba 2 mwaka huu
ni Mgambo Shooting vs Coastal Union, Tanzania Prisons vs Oljoro JKT, Azam vs
Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar vs Rhino Rangers na Mbeya City vs Ashanti United.
Raundi ya 13 ni kama
ifuatavyo; Novemba 6 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs
Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar. Novemba 7 mwaka huu ni Azam vs Mbeya City.
Ambapo aliongeza kuwa mechi za kufunga raundi ya 10 zitachezwa
kesho kama ratiba inavyoonesha ambapo mechi
hizo ni kati ya Coastal Union vs Simba, Tanzania Prisons vs Kagera Sugar na
Yanga vs Rhino Rangers.
No comments:
Post a Comment