Na Fatuma Rashid
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya watani wa jadi Simba na Yanga
iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3, imeingiza
sh.milioni 500,727,000.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Boniface Wambura alisema kuwa katika mechi hiyo mashabiki walikuwa ni
57,422 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 63 kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Wambura alisema kuwa
tiketi 131 hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C
ambapo tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi
ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo.
Alisema kuwa mapato
hayo yaligawanywa ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. milioni 123,025,564.32
wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75.
Wambura aliongeza kuwa mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia
15 ya uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh.
37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh.18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 14,596,253.39.
No comments:
Post a Comment