Na Mwajuma Juma, Zanzibar
Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi
Zanzibar, imekamata tani 205 za mchele mbovu na dawa zilizopitwa na muda kwa
matumizi binadamu.
Hayo yamebainishwa na
Mrajisi wa Bodi hiyo, Dkt. Burhan Simai, alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Mnazi Mmoja wilaya ya mjini Unguja. Alisema kati ya tani
hizo 205 mchele mbovu, tani 130 zimeingizwa nchini na kampuni ya UTS RICE
kutoka Pakistan na tani 75
zimeingizwa na kampuni ya Inter Link kutoka Kenya.
Dkt. Simai alisema kwamba
bidhaa hizo zilifanikiwa k u k ama twa kutokana na operesheni maalumu
iliyofanywa na Bodi hiyo hivi karibuni na kukamata tende tani 3.4 zilizotoka Dubai. Akizungumza na
waandishi wa habari alisema bidhaa zote hizo zinafanyiwa utaratibu wa
kuangamizwa na baadhi kurejeshwa zilizotoka kwa gharama za wamiliki wa bidhaa
husika
Sambamba na hilo alisema kuwa kumejitokeza tabia kwa
baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa hawahifadhi vyema bidhaa zao na
matokeo yake kuharibika mapema.
Kuhusu uingizwaji wa dawa feki
hapa nchini Mrajisi huyo alisema kwamba wameweka mtandao maalumu wa kuweza
kugundua dawa hizo na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika. Alisema kuwa
wakati wa kusimamia sheria umefika kwani wa fanyabiashara wengi wamekuwa
wakifanya udanganyifu kwa masilahi yao
binafsi bila ya kujali afya za watumiaji.
No comments:
Post a Comment