- WASITISHA MAANDAMANO,WAKUBALI MEZA YA MAZUNGUMZO
- JUKWAA LA KATIBA LAWAPA WOSIA,LATAKA WAWE NGANGARI
Na Mariam
Mziwanda
Vyama vitatu vya siasa
vinavyoshirikiana katika muungano wa kushinikiza k utokusaini wa kwa Muswaada
wa Katiba vimeridhia kukutana na Rais Jakaya Kikwete, pamoja na kusitisha
maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kesho.
Wakati viongozi hao
wakifikia uamuzi huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, ametaka
viongozi wa vyama hivyo watakapoenda kuonana na Rais Kikwete, kutokuwa wepesi
na ahadi watakazoahidiwa na kiongozi huyo wa nchi badala yake wawe ngangari
kusimamia hoja za msingi.
Kauli hiyo ya Kibamba inatokana na viongozi wa vyama hivyo vya
CUF, NCCR-Mageuzi na CHADEMA kutangaza kuwa wapo tayari kukutana na Rais
Kikwete, walipozungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana.
Mkutano wa viongozi hao ulifanyika Makao Makuu ya NCCR-Mageuzi,
ambapo Mwenyekiti wa viongozi hao, Prof Ibrahim Lipumba, aliwaambia waandishi
wa habari kuwa kutokana na taarifa walizopata kupitia vyombo vya habari kuwa
Rais Kikwete, yupo tayari kukutana nao wameona ni busara kuahirisha michakato
ya kisiasa.
Prof. Lipumba alisema Rais Kikwete ameonesha busara ya kuhitaji
mazungumzo. ”Tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari na mitandao na
tumekubali kuwa tayari endapo Rais anahitaji mazungumzo, basi tuzungumze naye
hivyo tunatoa taarifa kwa umma kuwa tunasitisha maandamano ambayo maandalizi
yake yalikuwa yamekamilika ambayo yalikuwa yaanze Oktoba 10 (kesho) hadi
tutakapokutana na Rais,” alisema.
Aliongeza kuwa wakiwa
wanasubiri mazungumzo hayo na Rais Kikwete ambayo yatajadili mustakabali wa
Katiba Mpya, kupitia Umoja wao wanamshauri Rais Kikwete kuwa ni busara asisaini
Muswada huo ili kuondoa kasoro zilizopo na kufanya majadiliano.
Walisifu muda ambao Rais Kikwete amepanga
kukutana nao ambao ni kati ya Oktoba 13 na 15. "Huu ni muda mwafaka
katika kupata mchakato wa Katiba Mpya unaoheshimu matakwa ya wananchi na
muungano wa nchi mbili kutokana na umuhimu wa jambo hilo," alisema.
Akizungumza kwa kina hatua
hiyo ya vyama vya upinzani, Kibamba alisema kuwa katika mazungumzo ya awali
kati ya ofisi yake na viongozi hao, Jukwaa lilishauri juu ya umuhimu wa kukutana
na Rais Kikwete iwapo nafasi hiyo ingetokea.
"Tuliwaambia
wasiichezee kwani itakuwa mwafaka badala ya maandamano ambayo yanatumia nguvu
nyingi," alisema na kuongeza;
"Nawasihi viongozi hao kutokuwa laini (wepesi) sana kwenye ahadi
watakazopewa na Rais badala yake kuwepo na makubaliano yenye hoja za msingi na
yanayotekelezeka kwa mahitaji ya Rais..hivyo ni lazima wawe ngangari,"
alisema.
Aliongeza kuwa wananchi
waelewe wanasiasa wanaangalia zaidi sanduku la kura na hoja zao huwa
hazifikirii wananchi waliopo vijijini hivyo viongozi hao ni muhimu kutambua
suala hilo.
“Hivyo nasisitiza wasije kutoka
Ikulu na makubaliano ya wingi wa nafasi za uongozi bungeni badala ya masilahi
ya Watanzania wote," alisema Kibamba.
hapo sawa
ReplyDeleteJK warudishe bungeni wakagaragazwe tena kwa kura. Hawana majority!!!
Delete