Na Mwandishi Wetu
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Ruvu Shooting
na Simba lililochezwa juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 75,692,000
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Boniface Wambura, watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo lililomalizika kwa
timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 13,395.
Alisema viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa
sh. 17,983,902.31 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
11,546,237.29.
Mgawo mwingine wa
mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,144,357.11, tiketi sh. 3,183,382,
gharama za mechi sh. 5,486,614.26, Kamati ya Ligi sh. 5,486,614.26.
"Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,743,307.13, Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,066,841.66 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,066,841.66," alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment