Na Fatuma Rashid
Timu ya taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Serengeti Boys), imealikwa kushiriki
Olimpiki ya Afrika itakayofanyika Mei mwakani.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF),
Boniface Wambura alisema soka ni kati ya michezo 22 itakayoshindaniwa katika
mashindano hayo , yatakayofanyika Gaborone,
Botswana chini
ya Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA).
Wambura alisema kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Tanzania
imepewa nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa Afrika,
kutokana na kuwa na programu nzuri za vijana hasa chini ya umri wa miaka 17.Alisema hiyo itakuwa ni michezo ya pili ya
Afrika kwa Olimpiki, ambapo ya kwanza ilifanyika mwaka 2010 jijini Rabat, Morocco.
No comments:
Post a Comment