03 October 2013

NIYONZIMA, TWITE HAKIJAELEWEKA YANGA



Na Nasra Kitana
    Wakati Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wakijiandaa na mchezo wa ligi hiyo kesho kutwa dhidi ya Mtibwa Sugar, nyota wao kiungo Haruna Niyonzima na beki Mbuyu Twite wameshindwa kujiunga na wenzao mazoezini.Timu hizo zitashuka Jumamosi katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kusaka pointi tatu muhimu.

    Tangu juzi, Niyonzima na Twite hawajajiunga na wenzao mazoezini kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola Mabibo, Dar es Salaam ambapo pia timu hiyo hufanya na mazoezi ya viungo ‘gym’ iliyopo Quality Centre. Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Ally alisema anachofahamu ni kwamba wachezaji hao wana matatizo ya kifamilia na ndiyo maana wameshindwa kujiunga na wenzao mazoezini.
   Hafidh hakuwa tayari kuanika matatizo ya wachezaji hao kwa madai ni siri yao na uongozi, hivyo vizuri kuweka hadharani matatizo ya mtu kwani watakuwa hawajawatendea haki.
 “Niyonzima na Twite wote wawili wana matatizo ya kifamilia na ndiyo maana wameshindwa kujiunga na wenzao,lakini wakiyamaliza wataungana na wenzao tena hivyo tunaimani tutakuwa nao kwenye mchezo wetu wa Jumamosi,” alisema. Awali ilidaiwa kuwa Twite, alikuwa ni mgonjwa, lakini daktari wa timu hiyo Nassoro Matuzya alipoulizwa kuhusu kuumwa mchezaji huyo, alisema hana taarifa zake.

No comments:

Post a Comment