Na Mwandishi Wetu, Aliyekuwa
Beijing, China
Wawakilishi mbalimbali wa asasi zisizo za kiserikali kutoka
nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, wamependekeza mbinu mpya za kuhakikisha
umaskini unapungua Afrika hususan Tanzania kama si kuondoka kabisa ili
kuharakisha maendeleo ya bara hilo.
Aidha,
wamependekeza kutenga fungu maalumu la fedha kwa ajili ya kukuza biashara za
ubia baina ya watu wa China na Afrika ili kuinua watu wenye kipato cha chini na
maskini. Mapendekezo
mengine ni pamoja na kuwa na utaratibu wa kubadilishana watu hususani wataalamu
mbalimbali ili kukuza mahusiano ikiwemo tamaduni za nchi hizo.
Wawakilishi hao
kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania, walitoa mapendekezo hayo
hivi karibuni katika kongamano la siku moja lililoandaliwa na Taasisi
Inayosimamia Shughuli Zote za Taasisi Zisizo za Kiserikali nchini China (CNIE),
katika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kimataifa cha Beijing (BFSU) mjini Beiging,
China.
Kongamano
hilo la wanazuoni lilihudhuriwa na wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka nchi
za Afrika na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kujadiliana namna ya
kufikia maendeleo ya pamoja na kuondokana na umaskini katika ushirikiano baina
ya nchi za Afrika na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini China, Fred Maiga aliishauri Serikali
ya China kuweka mkakati utakaohakikisha watu wa Afrika na Wachina
wanashirikiana ili kufikia maendeleo. "Maendeleo
ya mahusiano yalenge watu zaidi. Maendeleo katika mahusiano ya China na Afrika
yamewaleta watu wa mataifa hayo karibu. Mahusiano hayo yanapaswa kuangalia
zaidi uhusiano wa kibiashara na uelewa wa tamaduni za nchi hizo,"
alisisitiza Maiga katika hotuba yake.
Mbali
na hayo walipendekeza kubadilishana wataalamu pamoja na kutumia Umoja wa
Watanzania waliosoma nchini China katika kukuza na kutangaza umuhimu wa
uhusiano baina ya China na Tanzania ili kulenga kukuza ushirikiano.
"Wachina
ni wachapakazi sana ili kufikia ndoto yao ya 'Chinese Dream' (Ndoto ya
Wachina). Wachina wanaweza kushirikiana na Waafrika katika kukamilisha ndoto ya
Afrika ya umoja kwa kuungana, kushirikiana na kusaidiana ili kukamilisha ndoto
hizo," aliongeza Maiga.
Ndoto ya China ni dira
iliyozinduliwa na Rais wa China, Xi Jinping ambaye alitembelea Tanzania ikiwa
ni nchi ya kwanza Afrika na ya pili duniani wiki chache baada ya kuteuliwa kuwa
rais wa taifa hilo mwezi Machi, mwaka hu
No comments:
Post a Comment