- MOTO WATEKETEZA NYUMBA YAKE
Kiungo wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima amepata pigo
kubwa baada ya jana kuunguliwa na nyumba yake iliyopo maeneo ya Magomeni
Makuti, Dar es Salaam
.
.
Kwa mujibu wa
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Ally ambaye alikuwa katika eneo la tukio alisema
moto huo ulisababishwa na shoti ya umeme na kusababisha hasara kubwa kwa
mchezaji huyo.
"Kwakweli
nipo hapa eneo la tukio baada ya kupata taarifa za mchezaji wetu kuunguliwa na
nyumba, tunashukuru Mungu majirani walijitokeza kwa wingi na kusaidia kuuzima
moto huo ambao tayari ulikuwa umeshaleta hasara kubwa," alisema Hafidh.
Alisema moto huo uliibuka sebuleni kwa mchezaji huyo na kuteketeza
fenicha zote zilizokuwepo ikiwemo na laptop, lakini thamani halisi ya vitu
vilivyoungua haijajulikana kwa kuwa ni vitu vingi vilivyoteketea kwa moto.
Inadaiwa kuwa, janga hilo lilitokea
wakati mchezaji mwenyewe akiwa ndani ya nyumba hiyo na kama
si jitihada za majirani kujitokeza kumsaidia kuuzima moto huo, athari ingekuwa
kubwa zaidi.
Imeelezwa kuwa nyumba hiyo ina wapangaji wawili na upande ulioathirika
kwa moto ni ambao anaishi mchezaji huyo. Mchezaji huyo amekumbwa na tukio hilo ikiwa ni siku moja
tu, tangu adaiwe kuwa anashindwa kuripoti mazoezini kutokana na kukabiliwa na
matatizo ya kifamilia yeye pamoja na beki Mbuyu Twite.
No comments:
Post a Comment