Na Mwandishi Wetu
Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC) imezindua rasmi promosheni ya muda wa miezi mitatu ya kuweka
akiba iitwayo 'Weka Upewe' itakayogharimu zaidi ya sh. milioni 300.Promosheni
hiyo ina lengo la kuhamasisha wateja wake nchi nzima kuwa na utamaduni wa
kujiwekea akiba ikiwa ni moja ya matukio ya kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa
Wateja wa NBC
. Akizungumza na
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya benki hiyo,
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Mwinda Kiula Mfugale alisema kwamba,
benki hiyo ipo katika kipindi cha kufurahi na wateja wake, kwa kuonesha umuhimu
wao kwa kuwaunga mkono katika kipindi chote cha huduma zao nchi nzima.
"Kampeni hii si tu ina nia ya kufurahi na
wateja wake kwa kuwaunga mkono, lakini pia kuwafanya wateja wawe na utamaduni
wa kutunza na kujiwekea akiba kwa manufaa ya baadaye."Tunatarajia kwamba
wateja wetu watajitokeza kwa wingi katika kuweka akiba katika Akaunti ya
Malengo na Amana Maalum, ambapo watajishindia zawadi mbalimbali kama vile pikipiki, jenereta na gari aina ya Suzuki
Swift," alisema.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Masawe
alisema kwamba wateja wa benki hiyo kupitia promosheni hiyo wataweza kujifunza
kuweka akiba kwa maisha ya baadaye."Kutokana na mazingira ya sasa ya
kiuchumi ni muhimu kwa wateja wetu kujifunza namna ya kuweka akiba na matumizi
bora ya fedha ikiwemo kuwa na bajeti katika maisha yao ya kila siku," alisema.
Katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya
promosheni watapatikana washindi sita ambao watajishindia jenereta, pikipiki na
gari. Na ili mteja awe mshiriki ni lazima mteja afungue Akaunti ya Malengo au
ya Amana ya Malengo ambayo ni ya mwaka mmoja, lakini pia promosheni hiyo
inaweza kuwanufaisha wateja wapya.
No comments:
Post a Comment