Na Juma Kiyenze
.
Mzee Rashid
Mfaume Kawawa ‘Simba wa Vita’ ni mwanasiasa mkongwe alisimamia kikamilifu
utekelezaji wa majukumu ya Serikali aliyokabidhiwa kwa nidhamu, uadilifu na
bila woga hapa nchini.Hakika alikuwa ni miongoni
mwa viongozi wachache wazalendo, jasiri na mhimili mkubwa wa Hayati Mwalimu
Julius Nyerere, wakati wa harakati ya kupigania uhuru wa Tanganyika
dhidi ya Wakoloni wa Uingereza.
Alikuwa Waziri Mkuu wa
kwanza wa Serikali ya Tanganyika
mwaka 1962 na Tanzania
1972 hadi 1977, Makamu wa Pili wa Rais na Waziri wa Ulinzi na JKT 1977 mpaka
1980.Alizaliwa Mei 27, mwaka
1926 Kijiji cha Matepwende, Tanganyika na alifariki Desemba 31, 2009 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka
83. Watanzania wanamkumbuka
Mzee Kawawa kutokana na harakati zake katika utekelezaji wa majukumu ya chama
na Serikali kitaifa na kimataifa hapa nchini.
Uanzishwaji
wa JKT
Mzee Kawawa alisimamia
kikamilifu uanzishwaji wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Julai 10 mwaka 1963,
baada ya kufanyika uamuzi sahihi wa viongozi.K u a n z i s h w a k w a k
e kulitokana na mawazo ya Marehemu Mzee Kawawa ‘Simba wa Vita,’ baada ya
kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Bi. Gold Meir, katika
sherehe za uhuru nchini Ghana.
‘Simba wa Vita,’ alikuwa
nchini humo akiwakilisha Chama cha Wafanyakazi wa Tanganyika (TFL), akifuatana na
Mwalimu Nyerere kwa tiketi ya Tanganyika African National Union (TANU).Kiongozi huyo wa Israel, ambaye
aliwahi kuwa Waziri Mkuu nchini humo, alimwalika Mzee Kawawa kwa chakula cha
jioni, ambapo walipata fursa ya kuzungumza umuhimu wa JKT na jinsi vijana
wanavyoandaliwa kutumikia nchi yao kwa uzalendo, uadilifu, moyo na nidhamu
katika suala zima la malezi.
Mzee Kawawa alirejea h o t
e l i n i , a l imwe l e z a Mwalimu Nyerere, kuhusu mkutano wao na jinsi Israel
wanavyowaandaa vijana kutumikia taifa lao kwa njia ya kujitolea.A l i p o r u d i n c h i n
i Tanganyika, mawazo yake aliyapeleka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa
Chama cha Tanganyika African National Union (TANU Youth League), Hayati Joseph
Nyerere, ambaye aliyafikisha katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika
mkoani Tabora Agosti 25,1962.
Mkutano huo uliafiki mawazo ya viongozi hao na
Aprili 19, 1963, Baraza la Mawaziri la Tanganyika
chini ya Rais wa Jamhuri ya Tanganyika,
Mwalimu Nyerere, lilipitisha azimio la umoja huo.
Mnamo Julai 10, 1963 JKT ilianza kutekeleza
majukumu yake kwa kuwachukua vijana kutoka mikoa mbalimbali ya nchi kujiunga na
jeshi hilo na
kundi la awali la vijana 11 kutoka wilaya 11 walipata mafunzo Kambi ya JKT
Mgulani Dar es Salaam.
Kuanzishwa kwa chombo hicho, kulilenga umoja wa
kitaifa, kuwapatia mafunzo ya kijeshi na stadi za maisha vijana waweze
kulitumikia taifa lao kwa ukakamavu na uzalendo katika nyanja mbalimbali za
uchumi, jamii, kilimo, ulinzi na usalama wa taifa.
Malengo mengine yalikuwa ni kujenga mshikamano,
udugu, kujitegemea, kuongeza ufanisi wa kazi, nidhamu, kujituma na kuwaandaa
vijana kulitumikia taifa kupitia sekta binafsi na vyombo vya ulinzi na usalama
kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
JKT ilifanikiwa kutimiza malengo yake kitaifa na
kimataifa kuwakomboa wananchi kiitikadi, kielimu, kisaikolojia, kiutamaduni,
kiutendaji na kwamba hakukuwa na ubaguzi ulioruhusiwa kuota mizizi miongoni mwa
jamii.
Wananchi walijenga imani kubwa kwa JKT kulingana na
utendaji kazi wake kwa kujali jamii katika masuala ya maafa, kujitolea katika
mambo mbalimbali, ikiwamo ufundishaji wa elimu ya watu wazima, ujenzi wa makazi
na uelimishaji umma dhidi ya magonjwa, kilimo na utunzaji mazingira.
Msaada wa mafunzo kutoka Israeli
Itakumbukwa kwamba Serikali iliomba nchini Israeli
kuwafunza viongozi kuhusu uendeshaji wa JKT, ambapo mwaka 1960, baadhi ya
vijana walipelekwa nchini humo.
Miongoni mwao walikuwa ni aliyewahi kuwa Mkuu wa
JKT, Marehemu Meja Jenerali Makame Rashid Nalihinga, Brigedia Jenerali
(mstaafu) Dismas Msilu na Marehemu Brigedia Jenerali Irungi Athumani Msonge.
Pamoja na Israeli kuleta wataalamu wake hapa nchini
kwa ajili ya utoaji mafunzo zaidi, Serikali ilipanua wigo kwa kupeleka vijana
katika nchi za Bulgaria na Yugoslavia
kujifunza mbinu mbadala kuhusu suala zima la malezi.
JKT ilipoanza kutekeleza majukumu yake, iliwachukua
vijana wa kujitolea kutoka mikoa mbalimbali ya nchi na baadaye wasomi kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mujibu wa sheria.
Mwandishi wa makala hii, alipata fursa ya
kuzungumza na Mzee Kawawa nyumbani kwake kijijini Madale mwaka 2006, enzi ya
uhai wake, ambapo anasema, vijana wasomi waligoma kwenda JKT kwa kutofahamu
umuhimu wake na waliandamana.
Pamoja na Bunge la Tanzania kuridhia wasomi kwenda JKT
mwaka 1967, Mwalimu Nyerere alitetea uamuzi wa Serikali wa kuridhia mafunzo
hayo, hivyo vijana waliokaidi amri hiyo walirejeshwa kwa wazazi wao kutafakari
kitendo chao cha kugoma.
‘Simba wa Vita’ anakumbuka jinsi Bw.Ali Said
Mchumo, baada ya kuhitimu elimu yake Chuo Kikuu alimfuata akiomba apelekwe JKT
akajitolee.
Kijana huyo ambaye aliwahi kushika nyadhifa
mbalimbali s e r i k a l i n i , a l i t a k i w a kuthibitisha kauli yake kwa
kuja na wazazi wake, am waliridhia mtoto wao aende JKT.
An a s ema , b a a d a y a kuthibitika alikwenda
kumpa taarifa Mwalimu Nyerere kuhusu ujasiri aliouonyesha kijana huyo, ambao
uliridhiwa na viongozi hao na alikubaliwa kujiunga na jeshi hilo akamilishe
dhamira yake.
Mzee Kawawa alijiunga JKT
Ilikuwa ni mwaka 1967, Mzee Kawawa na viongozi
wenzake walifanya uamuzi sahihi kujiunga na JKT Kambi ya Ruvu mkoani Pwani,
wakionyesha mfano, jambo ambalo haikuwa rahisi kutokana na uzito wa majukumu yao kitaifa.
Licha ya kukutana na mikasa mbalimbali jeshini,
alifikia uamuzi huo kutokana na umuhimu wa taasisi hiyo kwa manufaa ya taifa,
kwani kila mtu alipaswa kupitia mafunzo ya JKT kabla ya kuajiriwa katika sekta
ya umma ama binafsi.
Aliwataja viongozi hao kuwa ni pamoja na Waziri
Mkuu, Marehemu Edward Moringe Sokoine, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi na Chifu Adamu
Sapi Mkwawa.
“Tulipofika mlangoni, ilibidi tusahau vyeo na
madaraka yetu wakati ule, tulibeba mizigo yetu, tulipiga kwata na mazoezi
mbalimbali ya kijeshi kama tulivyotakiwa na
makamanda wetu,” anafafanua.
“Makamanda wale walikuwa wachungu, hawasikii wala
kujali umbile wala cheo cha mtu, wao walijali nidhamu na kufuatwa kwa
maelekezo,” anaeleza Mzee Kawawa.
Anasema kuwa, awali alipoingia Kambi ya JKT Ruvu,
akiwa na nywele nyingi, aliambiwa azikate mwanajeshi hatakiwi kuwa nazo, hali
iliyosababisha kamanda mmoja wa kike kuzikata kwa mkasi bila ya huruma, hivyo alitii
amri hiyo.
“Mimi enzi ya ujana wangu nilipendelea sana kufuga nywele ndefu
na sikuwahi kuzikata kwa kipindi cha mwaka mzima, sasa ghafla afande anazikata
bila ya huruma,” anasema.
Wakati anajiunga na JKT, Mzee Kawawa alihudhuria vipindi
mbalimbali bila ya kutoroka, hata alipokuwa anachelewa kwa udhuru makamanda
walimtafuta, hali iliyotokana na umaarufu wa nyadhifa zake za Makamu wa Pili wa
Rais na Waziri Mkuu wa Tanzania.
Hali hiyo ilimjengea heshima na uaminifu miongoni
mwa viongozi wenzake na makamanda wakati wa mafunzo na alikuwa mfano wa kuigwa
na wenzake.
Anaeleza kwamba, wakati fulani alichukua chupa ya
chai na kwenda nayo nyuma ya bweni lake
kujipatia stafutahi,
kabla hajamaliza alitokea afande aliyejulikana ‘Afande Ubwabwa,’ ambaye
aliamuru ampatie chupa hiyo.
Pamoja na kutii amri halali ya kiongozi wake, chupa
hiyo ilivunjwa mbele yake na kumwamuru haraka akajiunge na wenzake katika
foleni tayari kwenda porini kusenya kuni za kupikia.
Baada ya kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi, Mzee
Kawawa alipelekwa Kijiji cha Kitaya Mkoani Ruvuma kuimarisha ulinzi mpaka kati
ya Msumbiji na Tanzania.
Kudumishwa kwa ulinzi katika mpaka huo, kulitokana
na majeshi ya Ureno kuvuka mpaka mara kwa mara, hivyo kusababisha uharibifu wa mali na
usumbufu kwa wananchi.
Anaeleza Mzee Kawawa kuwa, akiwa huko, alikutana n
a Mk u u wa Ma j e s h i (mstaafu), Jenerali Sam Hagai Sarakikya, ambaye
aliwaeleza hali tete ya usalama mpakani, hivyo walitakiwa kuchukua tahadhari.
Akiwa askari alijiamini hasa baada ya kukabidhiwa
bunduki na risasi za moto tayari kukabiliana na adui, ingawa jeuri yao ilivurugwa na mnyama
kiboko aliyekivuruga kikundi chao.
Alikuwa ameweka risasi chemba tayari kwa kupiga
bila ya kuangalia usalama mbele yake, Jenerali Sarakikya alitoa amri kuwataka
askari waliokuwa nyuma kutofyatua risasi, licha ya mnyama huyo kuuawa na askari
aliyekuwa mbele yake.
JKT muhimu kwa malezi
“JKT imefanya mambo mengi mazuri katika kujenga
taifa letu, ambapo limepata sifa kubwa ndani na nje ya Bara la Afrika kutokana
na mshikamano na umoja wetu,” anasisitiza.
Anasema hatua mbalimbali zilizochukuliwa na
viongozi waasisi wa taifa letu chini ya Mwalimu Nyerere kupiga vita tabia zenye
kujenga chuki, kuleta mgawanyiko, tofauti ya kipato, elimu, jinsia, kabila na
dini ni lazima zidumishwe.
Pamoja na mafunzo ya JKT kusimamishwa mwaka 1994 na
kurudishwa tena mwaka 2001, ilikuwa ni hatua muhimu kuendeleza mazuri
yaliyoachwa na waasisi wetu kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo waweze
kufahamu tulikotoka, tulipo na tuendako bila ya kurubuniwa na mataifa mengine
kifikra, kiuchumi, kielimu na kisiasa kuleta uvunjifu wa amani nchini
No comments:
Post a Comment