Na Rachel Balama
Serikali imeshauriwa kufuta malipo ya vibali vya
kazi kwa walimu wanaotoka nje ya nchi ili kuzisaidia shule hizo kutoa elimu
bora na kutoathiri mapato na matumizi ya shule husika. Mwito huo ulitolewa Dar
es Salam, mwishoni mwa wiki na aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu, Joseph Mungai,
katika mahafali ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ghomme
ya Jijini.
Alisema kuwa serikali imekuwa ikiziteka shule binafsi zinazoajiri
walimu toka nje ya nchi dola 1,500 kwa ajili ya vibali vya kufanya kazi hapa
nchini. "Gharama kwa sasa zimepanda kutoka dola 4,000 kipindi cha nyuma
hadi kufikia dola 1,500, gharama ambazo ni mzigo kwa shule hizo," alisema.
Alisema kuwa ni vyema Serikali ikafuta gharama hizo kwa nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki ili shule zenye uwezo wa kuajiri walimu toka nje waweze
kuajiri na kutoa elimu bora. Aliongeza kuwa pia katika operesheni ya kuwaondoa
wahamiaji haramu maarufu kama operesheni
kimbunga, aliitaka serikali isiwakamate na kuwarudisha kwao walimu kutoka nchi
nyingine.
Alisema ni vyema Serikali ikawawekea utaratibu mzuri wa kurekebisha
vibali vyao vya kazi kwa walimu hao ili waweze kufundisha katika shule
mbalimbali hapa nchini.
Pia aliongeza kuwa Serikali iwe na wepesi wa kuzisaidia
shule binafsi kwa kuwa inao uwezo na pia ni wajibu wa serikali kuzisaidia shule
hizo. Katika mahafali hayo Mkurugenzi wa Benki ya Habib Afrika Limited, Syed
Mukhtar, alitoa vyeti na zawadi kwa wahitimu 62. Naye, mmiliki wa shule hiyo,
Emmanuel Malangalila, aliwataka wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wao
wanaomaliza kidato cha nne wanajiendeleza na kozi ndogo ndogo wakati wakisubiri
majibu yao.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi, George Mlawa, alisema kuwa katika dunia ya
sasa hauwezi kupambana na umaskini kama elimu
haizingatiwi. Alisema kuwa hakuna umaskini mbaya kama
wa mawazo ambao unatokana na watu kukosa elimu.
No comments:
Post a Comment