- MAWAZIRI ZANZIBAR,BARA SASA KUKUTANA
- KUJADILI MITAALA MASOMO YA DINI,MUZIKI
Na Faki
Mjaka-(MAELEZO) Zanzibar
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imesema masomo ya
dini na mengine, yataendelea kufundishwa pamoja na kufanyiwa mitihani katika
ngazi zote.
Alisema wizara
hiyo haijakubaliana na waraka wa elimu kutoka Tanzania Bara wa kuyafanya masomo
hayo kuwa ya hiari, hivyo yasichangie asilimia yoyote katika ufaulu wa
mtahiniwa.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Abdallah Mzee, ameyasema hayo Zanzibar jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari ili kukanusha taarifa zilizotolewa na baadhi
ya vyombo vya habari zikidai Wizara hiyo imeondoa mtaala wa masomo ya dini na
Kiarabu kwenye mitihani ya Taifa.
Alisema
watendaji kutoka Wizara ya Elimu Tanzania Bara, walikutana na wenzao wa Zanzibar ili kujadili
waraka wa elimu waliokuja nao uliokuwa unataka kufanyike mambo mapya.Bw. Mzee
aliongeza kuwa, katika waraka huo wenzao kutoka Bara walipendekeza masomo ya
dini ya Kiislamu, Kikristo, lugha ya Kiarabu, Kifaransa, Kompyuta, muziki yawe
ya hiari kwa mwanafunzi kuyasoma na yasisaidie ufaulu wowote katika viwango vya
madaraja ya ufaulu.
"Waraka
ulipendekeza masomo hayo yakiwemo dini na Kiarabu yasisaidie chochote katika
kupandisha au kushusha vision ya mtahiniwa," alifafanua Bw. Mzee. Aliongeza
kuwa, ilipendekezwa utaratibu huo mpya uanzwe kufanyiwa kazi kwa wanafunzi ambao wataingia kidato cha kwanza mwaka 2014 na ifikapo 2017, wanafunzi
hao wautumie katika kidato cha nne.Hata hivyo, Bw. Mzee alisema watendaji wa Zanzibar waliupinga utaratibu huo kwa kuwa haukidhi
matakwa ya Zanzibar.
"Watendaji
wetu waliupinga waraka huo kwani hautufai na unatofautiana sana na sisi kulingana na hoja zetu
tulizotoa, pia walikubali kuurudisha ili usiweze kufanyiwa kazi," alisema.
Alisema Wizara ya
Elimu Zanzibar, inatoa Mchepuo wa Masomo ya lugha katika skuli tofauti ikiwemo
Sekondari ya Kiponda hivyo itakuwa vigumu kufuata utaratibu huo.
Akizungumzia somo la dini, Bw. Mzee alisema
soko hilo kwa Zanzibar ni muhimu sana pia ni miongoni mwa masomo yenye walimu
wazuri wa ngazi za Stashahada hadi Udaktari-PhD na ufundishwaji wake huanzia
darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu hivyo kubadili utaratibu isingewezekana.
Aliongeza kuwa, katika dunia ya sasa, somo
kama kompyuta ni muhimu sana
hivyo kulifanya halina ulazima ni kujirudisha nyuma kimaendeleo."Licha ya
uhusiano mzuri uliyopo kati ya Wizara yetu na Bara, sisi hatukushirikishwa
katika uanzishwaji wa waraka husika," alisema.Katika hali ya kuliweka sawa
jambo hilo, Mawaziri wa Wizara hizo Bw. Ali Juma
Shamhuna na mwenzake wa Bara, Dkt. Shukuru Kawambwa, wanatarajia kukutana kesho
kulijadili jambo hilo
No comments:
Post a Comment