Mahakama ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, imemhukumu
mfanyabiashara maarufu mjini humo, Bw. Dola Jamal, kifungo cha miezi sita
gerezani kwa kosa la kumshambulia Mtawa wa Kanisa la Katoliki, anaripoti
Raphael Okello, Musoma
Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Faisal Kahamba ilidaiwa
na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Jonas Kaijage kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 10, 2010.
Alisema
siku ya tukio, mshtakiwa alimshambulia kwa vipigo na matusi Mtawa huyo (jina
linahifadhiwa) na kusababisha uvunjifu wa amani kwenye jamii.
Baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo, Hakimu Kahamba alitoa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela na
kutozwa faini ya sh. 500,000 ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Wakati huo huo, mahakama hiyo juzi ilimhukumu kifungo cha maisha mkazi wa
Nyakanga, wilayani Butiama, Nyamhanga Magesa (35) kwa kosa la kuchoma nyumba
tatu za mama yake mzazi, Nyangi Waryoba.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya
ya Musoma, Emmanuel Ngigwana, ilidaiwa na Mwendesha Mashtata wa Polisi, Theofil
Mazuge kuwa, mshtakiwa alivunja kifungu namba 319(a) cha kanuni ya adhabu sura
ya 16.
No comments:
Post a Comment