- SAFARI MIKOANI KUKWAMA,MIZIGO KUTOBEBWA
Na Goodluck
Hongo
Siku moja baada ya Chama cha Wamiliki wa Malori nchini (TATOA),
kutangaza usimamishaji huduma za kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi
kuanzia leo, Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA), nacho
kimetangaza usitishaji huduma zake (kusafirisha abiria), kuanzia kesho
. Awali TATOA
kilidai, lengo la kusitisha huduma ni kupinga agizo la Serikali kupitia Waziri
wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli kuondoa msamaha wa tozo ya uzito wa magari
yaliyozidi asilimia tano ya uzito unaokubalika kisheria.
Msemaji wa
TATOA, Bw. Elias Lukumay, alisema msamaha huo ulitolewa na Serikali mwaka 2006
baada ya kamati ambayo iliundwa na Serikali ikishirikisha kufanya ziara katika
mizani na kubaini haziko sawa kwa maana ya kutofautiana vipimo vyake.
Sababu
nyingine iliyosababisha Serikali kutoa msamaha huo ni ubovu wa barabara, matuta
mengi yaliyosababisha kuyumba kwa mzigo na mizani kutofanyiwa matengenezo.
Alisema uamuzi
huo wa Serikali haukuishirikisha TATOA kama ilivyofanya mwaka 2006 mbali ya
umuhimu wa sekta hiyo nchini hivyo ili kuepusha mgogoro na Serikali pamoja na
wafanyakazi wa mizani, wamekubaliana kupaki magari yao.
Wakati TATOA
ikitoa msimamo huo ambao utekelezaji wake unaanza leo, TABOA nao wamemtaka Dkt.
Magufuli kurudisha msamaha wa asilimia tano vinginevyo wanasitisha huduma za
kusafirissha abiria kwenda mikoa mbalimbali nchini pamoja na nje ya nchi
kuanzia kesho.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TABOA,
Enea Mrutu, alisema kitendo cha kuondoa asilimia tano kutayafanya mabasi mengi
kusafiri na abiria wachache hivyo wamiliki wake kuingia hasara.
Alisema tangu kutolewa kwa taarifa hiyo,
kumekuwa na misururu mikubwa ya magari katika mizani hivyo kusababisha usumbufu
mkubwa kwa abiria na kumaliza safari zao muda mbaya.
"Tunamuomba Dkt.
Magufuli arudishe msamaha wa asilimia tano aliouondoa, upo uwezekano mkubwa wa
mabasi kusafiri na abiria wachache hivyo kuingia hasara," alisema.
Alimtaka Dkt. Magufuli na Waziri wa Uchukuzi
Dkt. Harrison Mwakyembe, kutafakari uamuzi huo kwa kina ili kutoka na jawabu la
kurudisha msamaha huo kwani sekta hiyo inategemewa na wananchi wengi
wanaosafiri kila siku.
"Tumekuwa
hatushirikishwi katika masuala kama haya,
kitendo cha Serikali kuyaruhusu magari aina ya Noah yenye thamani ndogo kubeba
abiria zaidi ya uwezo wake pia hatukushirikishwa," alisema.
Wakati huo huo, Bw. Mrutu aliwataka wamiliki wote wa mabasi kufika katika Ofisi za
TABOA ili kuchukua fomu kwa ajili ya kupunguziwa bima kwa asilimia tano.
Aliwataka
na wamiliki ambao hawajajiunga na TABOA,wafanye hivyo sasa ili waweze
kushirikiana katika mambo muhimu yanayohusu huduma wanayoitoa kwa abiria
No comments:
Post a Comment