Jeshi la Ulinzi la
Wananchi Tanzania (JWTZ), limesema askari wake Luteni Rajabu Mlima, ameuwawa
mjini Goma, Congo (DRC), baada ya kupigwa risasi wakati akitekeleza jukumu lake
la ulinzi wa amani nchini humo, anaripoti Darlin Said.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari, ilisema Luteni
Mlima alipigwa risasi na kufa Agosti 27 mwaka huu, mjini Goma.
“Tukio hilo lilitokea wakati wa mapambano kati ya jeshi la
Serikali ya Demokrasia ya Congo
na waasi wa M23,” ilisema taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa, Luteni
Mlima akiwa na kikundi cha JWTZ kilichopo mjini humo, kilikuwa kinakwenda
kukinga raia wasidhurike na mapigano hayo katika eneo la Kiwanja, kwenye Milima
ya Gavana, nchini humo.
No comments:
Post a Comment