- AKIRI WAKULIMA KUDAI BILIONI 17/- ZA MAHINDI
- KUTOA MELI ZIWA NYASA , VICTORIA, TANGANYIKA
Na Mwandishi Wetu,
Ludewa
Rais Jakaya Kikwete, amesema ni aibu
Serikali kudaiwa na wakulima wa Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe ambao wameiuzia
mahindi yao. Kutokana
na hali hiyo , aliwahakikishia wakulima hao kulipwa fedha zao haraka
iwezekanavyo.
Rais Kikwete
aliyasema hayo juzi kwa nyakati tofauti wilayani humo ikiwa ni mwendelezo wa
ziara zake za kukagua, kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.“Ni kweli
Serikali inadaiwa sh. bilioni 17 ambazo ni deni la wakulima wa mikoa mbalimbali
nchini ambao walituuzia mahindi yao
msimu uliopita kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),” alisema.
Akipokea
Ripoti ya Maendeleo wilayani humo, Rais Kikwete alisema wakulima wa Wilaya hiyo
pekee bado wanaidai serikali sh. bilioni 3.115 za mahindi tani 6,231
waliyoyauza NFRA.Alisema hadi sasa
wakulima wilayani humo wamelipwa shilingi bilioni 2,839 zilizotokana na tani 5,679
za mahindi ambapo NFRA ililenga kununua tani 13,000 lakini imeweza kununua tani
11,911 ingawa sehemu kubwa ya kiasi hicho hakijalipiwa na Serikali.
“Hii ni aibu, Serikali haiwezi kudaiwa na
wakulima hivyo hizi fedha zitalipwa tu,” alisema Rais Kikwete na kuelezea hatua
binafsi alizochukua kuhakikisha deni hilo
linalipwa.Aliongeza kuwa, Serikali itaangalia uwezekano
wa kununua tani 2,972 za mahindi ya msimu uliopita zilizobakia mikononi mwa
wakulima wa Wilaya hiyo.
“Nimeambiwa NFRA bado inahitaji tani 40,000,
ili kukamilisha shehena ya idadi ya tani 250,000 za mahindi kwa ajili ya
Hifadhi ya Taifa mwaka huu...nitawaambia waangalie kama
kuna uwezekano wa kununua tani zilizobaki kwa wakulima wa Ludewa,” alisema.
Rais Kikwete pia alizungumzia maombi ya
wananchi wa Ludewa kutaka Serikali inunue meli ili kuchukua nafasi ya Mv. Mbeya
iliyozama katika Ziwa Nyasa ili kurahisisha usafiri ndani ya ziwa hilo ambalo linapakana na
Wilaya hiyo.
Alisema Serikali itanunua meli kwa kwa ajili
ya usafiri katika Maziwa Makuu nchini, kabla ya mwaka 2015 na zinaweza kuwa
mbili badala ya moja katika Ziwa Nyasa,
Victoria, Tanganyika.
“Tunajua kuwa meli ya
Mv. Mbeya ilizama katika Ziwa Malawi
na nyingine katika maziwa mengine makubwa ya Tanganyika na Victoria...mimi
katika kampeni zangu niliahidi nitanunua meli moja kwa kila ziwa,” amesema Rais
Kikwete na kuongeza;
“Tumeagiza meli tatu kutoka Korea Kusini kwa
sasa zinajengwa, pia tumeagiza meli nyingine tatu kutoka nchini Denmark nazo
zinajengwa hivyo tunaweza kupata meli zaidi ya moja katika maziwa yote matatu
na mbili nitazizindua kabla ya kumaliza kipindi changu cha uongozi mwaka 2015,”
alisema.
Al isema kero nyingine zilizoibuliwa na
wakazi wa Wilaya hiyo pamoja na ujenzi wa daraja kwenye Mto Ruhuhu, litajengwa.
Wakati huo huo, Rais Kikwete amewaonya wananchi wa Wilaya hiyo wasiwe hodari wa
kuuza ardhi na mashamba yao
ambayo yatakuwa na umuhimu mkubwa miaka michache ijayo kutokana na matunda makubwa
ya uwekezaji.
Alisema Serikali inatarajia kuwekeza katika
miradi ya chuma, makaa ya mawe na madini mengi yanayopatikana wilayani humo..Rais
Kikwete aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo
na kusisitiza kuwa; Msipochangamka mapema na kuanza kuangalia namna ya
kunufaika na rasilimali za hapa, mtageuka ‘manokoa’ wa watu wengine kwenye
ardhi yenu wenyewe,” alisema Rais Kikwete a, wakulima wilayani humo wamelipwa
sh. bilioni 2.839 zilizotokana na tani
No comments:
Post a Comment