Aliyekuwa Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), mstaafu James
Kombe (pichani) amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali
ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam, anaripoti Frank Geofray-Jeshi la Polisi
Akizungumzia kifo hicho, Msemaji wa Jeshi la
Polisi Nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera Senso alisema, Kombe
alifariki hospitalini hapo jana ambapo taratibu za mazishi zinaendelea. Alisema
marehemu alizaliwa mwaka 1950, Mwika mkoani Kilimanjaro, alijiunga na Jeshi la
Polisi Machi 15,1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda,
kupandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.
Baadhi ya vyeo
alivyopitia na miaka aliyopata vyeo hivyo katika mabano ni Sajenti wa Polisi
(1973), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1977), Mkaguzi wa Polisi (1984) na Mrakibu
Msaidizi (1986).Vingine ni Mrakibu wa Polisi (1991), Mrakibu Mwandamizi (1995),
Kamishna Msaidizi wa Polisi (1998) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(2002), hadi alipostaafu mwaka 2010.
Baadhi
ya nafasi alizowahi kuzitumikia jeshini ni pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya
(OCD) katika Wilaya za Dodoma,
Tarime, Serengeti na Arusha pamoja na Kuwa Mkuu wa Polisi Mkoa (RPC) katika
mikoa ya Lindi, Arusha na Kigoma. Pia marehemu aliwahi kuwa Mkuu wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia nchini (FFU
No comments:
Post a Comment