Na Mwandishi Wetu
Mgombea wa nafasi
ya Ujumbe wa Shirikisho la Mpira w a Miguu Tanzania(TFF), Geofrey Nyange 'Kaburu'
kupitia Kanda nam ba 11 ya Morogoro na Pwani, amewataka wapiga kura katika Uchagu
zi Mkuu utakaofanyika Jumapili hii, kumchagua ili awez e kushirikiana na
viongozi wenzake kuleta mabadiliko kat ika taasisi hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaburu alisema anaomba wajumbew
amchagueili awezek ufanyiamaboresh ochangamo tombalimba lizasoka ndaniyanc hi
hii.Kaburu aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba pamoja na Mju mbe wa Kamati
ya Ligi ya Shirikisho hilo alisema, endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa mjumbe
atahakikisha anaendeleza soka la vijana kwanza ,ambalo litazaa wachezaji wazuri
wa timuzat aifa.
Alisema ana imani kubwa vijana kwa sasa wanakosa kipaumbele na ndiyo sa
babu kubwa ya timu ya taifa kufanya vibaya na kuporomoka kila kukic ha katika viwango vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) na endapo atapata nafasi hiyo, athakikisha vijana wanapewa nafasi kubwa ili baadaye Stars,iweze kuwa tishio.
"Endapo nitapata nafasi ya kuwa
Mjumbe kupitia kanda yangu ya Moro goro na Pwani kwa uwezo na jitihada kubwa niliyonayo katika kuendelez a michezo,nitaanzia kwanza kusimamia vijana kwa kushirikiana na wajumbe wenzangu,ambao nitafanikiwa kuwa nao endapo nitachaguliwa,"alisema
Kaburu na kuongeza kuwa,bila vijana haiwezekani kupata timu nzuri ya taifa..Kaburu alisema,pia atahakikisha anakuwa
bega kwa bega na wadau mbalimbali ambao wataisapoti soka izidi kukua, sambamba
na kusimamia timu za wanawake kwa kushirikiana na wajumbe wenzake, ili wanawake
waweze kupata hata ligi kama ilivyo kwa timu ya wanaume .
Alisema atasimamia masilahi ya waamuzi,
ili waweze kuwa na morali muda wote wawapo kazini kwa ajili ya kufanya kazi zao
kwa uadilifu mkubwa sambamba na kusimamia masilahi ya wachezaji katika klabu
zao ili wawe na morali, hata wakiitwa timu ya taifa waweze kuitumikia vyema.
"Kuna mambo mengi sana
ambayo nimepanga kuyafanya endapo nitaingia ndani ya shirikisho hilo kama Mjumbe, hivyo
basi nina imani kubwa wapigakura wanaujua uwezo wangu ulivyo katika kuongoza
soka hapa nchini na naamini kwa mawazo yangu na wajumbe wenzagu tutafika mbali
katika Soka hapa nchini," alisema Kaburu.
No comments:
Post a Comment