Na Ramadhan Libenanga, Morogoro
Mtangazaji mkongwe na aliyekuwa Meneja wa Kituo cha
Abood Media, mkoani Morogoro, Julius Nyaisanga kwa jina maarufu (Uncle J),
amefariki dunia jana saa moja asubuhi katika Hospitali ya Mazimbu, Manispaa ya
Morogoro
.Akizungumza na Majira,
Meneja Matangazo wa kituo hicho, Bw. Abed Dogoli, alisema marehemu Nyaisanga
alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Alisema taratibu za mazishi
zinafanyika nyumbani kwa marehemu Kihonda na atasafirishwa kwenda nyumbani kwao
mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.
Mke wa marehemu, Bi. Leah
Nyaisanga alisema mumwe alizidiwa juzi jioni na kupelekwa hospitalini hapo
ambapo kifo chake ni pigo kubwa kwa familia yao, wadau wa tasnia ya habari na Watanzania
kwa ujumla.
"Marehemu aliwahi
kufanya kazi kwenye Kampuni ya IPP, akiwa Mkurugenzi wa Radio One, awali
aliwahi kufanya kazi Radio Tanzania
wakati huo ikiitwa (RTD)," alisema..Mbunge wa Morogoro Mjini,
Bw. Aziz Abood (CCM), alisema amepokea taarifa za msiba huo kwa mshtuko mkubwa
kwani marehemu alijituma na kufanya kazi zake vizuri.
"Nilimfahamu marehemu
miaka mingi tangu akiwa kwenye vituo mbalimbali vya utangazaji na alikuwa
mahiri," alisema..Marehemu
Nyaisanga ameacha mke na watoto watatu ambao ni Samuel, Noela na Beatrice.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
No comments:
Post a Comment