- WADAI AMESHINDWA KUJENGA BARABARA URAMBO
Na Goodluck
Hongo, Urambo
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), kimesema kama kitapewa ridhaa ya
kuongoza nchi mwaka 2015, watabadilisha matumizi ya Ofisi ya Spika iliyojengwa
na mbunge wa Urambo Mashariki, Bw. Samuel Sitta.
Akizungumza
juzi katika mkutano wa hadhara wilayani humo, mkoani Tabora, Mkurugenzi wa
Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa, alisema ofisi hiyo
wataibadilisha kuwa wodi ya wazazi ili iweze kuwasaidia wanawake wanaoteseka
kupata huduma ya afya.
Alisema Bw. Sitta
alijenga jengo hilo ili litumike kama ofisi ya
Spika wa Bunge kabla ya kumaliza muda wake wakati mji huo hauna barabara za
lami wala hospitali za kutosha hivyo kama watapewa
ridhaa, watalibadili matumizi yake.
Alisema Mkoa huo una
historia kubwa nchini lakini hauna maendeleo ambapo badala ya Serikali kujenga
barabara nzuri na kuwapa wananchi maji safi
na salama, Bw. Sitta alijenga ofisi akiamini hata ondoka katika kiti hicho.
"Sitta amekuwa
mbunge tangu 1976 katika jimbo hili lakini hadi leo hakuna barabara za lami
mjini wala zinazoingia na kutoka katika jimbo hili," alisema Mtemelwa..Aliongeza kuwa, miaka
ambayo Bw. Sitta amekuwa mbunge wa jimbo hilo
inamtosha hivyo ni lazima wananchi wachague mbunge kutoka upinzani ambaye
hataogopa kusema ukweli ili kuharakisha maendeleo yanayohitajika.
Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi inayoundwa na Mikoa ya Katavi,Tabora na
Kigoma, Bw. Shabani Mambo, alisema kwa muda mrefu wakazi wa Kigoma walikuwa
wakikichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini walikosa maendeleo na baada ya
kuchagua upinzani, hivi sasa Kigoma imebadilika kwa kiasi kikubwa.
Alisema lazima
wananchi wawe na upeo wa kufikiria kwani Mkoa wa Tabora wenye majimbo tisa,
hakuna hata moja ambalo limechukuliwa na upinzani na matokeo yake hakuna
maendeleo..Aliwataka wananchi wa jimbo hilo kubadili uongozi uliopo kwani licha ya
Mkoa huo kubarikiwa Mawaziri, hadi leo hauna maendeleo ya kujivunia
No comments:
Post a Comment